ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 19, 2011

MISS LAKE ZONE KIKAZI NA KIJAMII ZAIDI.

Tukiwa na siku chache hatimaye siku itimu (23.JULY.2011) tupate kukishuhudia kinyang'anyiro cha miss lake zone 2011 warembo washiriki mwishoni mwa wiki walipata fursa ya kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea hospitali ya Sekou Toure iliyopo jijini Mwanza na kisha mengine yakafuata CHEKSHIA PICHAZZzzzz!Warembo wa Vodacom Miss Lake zone 2011 walishiriki kufanya usafi katika Hospitali ya mkoa ya Sekou Toure.

Mrembo Lydia Fredric akifanya usafi katika moja ya wodi za wazazi katika hospitali ya mkoa ya Seketoure

Warembo wa Vodacom Miss Lake zone 2011 wakifurahi kumbeba mtoto.

Mrembo Jackline Dismas akikabidhi Mche wa sabuni kwa Mama mjamzito katika moja ya wodi za wazazi katika Hospitali hiyo ya Mkoa.

Warembo wa Vodacom Miss Lake zone 2011 pia walipata fursa ya kutembelea soko la Kimataifa la Mwaloni jijini mwanza, hapa wanaonekena wakiuliza maswali juu ya biashara ya dagaa na samaki mwa kukaushwa sokoni hapo.

Warembo wa Vodacom Miss Lake Zone 2011, wakipata maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Mwaloni ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwaloni Mh. Novak Manoko mwenye shati jeupe.

Muongozaji kutoka Vodacom bi. Miriam, akitoa maelezo ya utendaji kazi wa ofisi ya Huduma za mawasiliano Vodacom Mwanza.

Baadaye Warembo wa Vodacom Miss Lake zone 2011 walielekea Kiwanda cha Bia TBL ambako walijionea shughuli mbalimbali za utengenezaji wa vinywaji vizalishwavyo na kampuni hiyo. Pichani wakiwa wamepozz na muandaaji wa shindano Bi. Clara.
Jumamosi ya tarehe 23 july 2011 nani kulinyakuwa taji?

Picha na THE BIG TOP TEN.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.