ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 5, 2011

OBAMA : PICHA ZA OSAMA HAZICHAPISHWI

Wakati dunia ikiwa na usongo kuhakiki na kuipata sura kamili ya mwili wa jamaa aliyesakwa zaidi kuliko wote ulimwenguni (Osama Bin Laden), Rais Barack Obama ameamua kuwa picha za Osama Bin Laden, aliyeuwawa siku ya jumatatu, zisichapishwe.

Maafisa wa Marekani wamekuwa wakijadili iwapo wachapishe picha za mwili wa Bin Laden kukabili habari za uongo kuwa hakuuawa.

Lakini Bw Obama anaamini kuwa picha hizo huenda zikazua hisia kali akisema, '' sisi hatutaki kuonyesha picha hizi kama kikombe cha kujivunia cha kumwonyesha kila mtu."


Waandishi wa habari sambamba na wananchi wamekuwa wakifuatilia kwa saa 24 eneo yalipokuwa makazi ya Osama.

Kiongozi huyo wa al- Qaeda alipigwa risasi katika uvamizi jumatatu iliyopita na vikosi maalum vya Marekani, Kaskazini mwa Pakistan. Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema kuwa rais Obama ameamua wazi kuwa kutoa picha hizo hazina thamani yeyote kwani huenda ikatishia maisha ya raia. Bw Obama amefichua uamuzi huo wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS.

Kutoka dirishani.
Uamuzi huo ulifikiwa wakati maafisa wa Marekani walianza kuchunguza habari kwenye kompyuta, simu za rununu na vifaa vingine vya kuhifadhi habari ambavyo vilipatikana wakati wa uvamizi huo katika eneo la Abbottabad, ambapo Bin Laden alikuwa amejificha.

Laini mbili za simu na euro 500 ($745; £450) zilipatikana zime shonelewa kwenye nguo ya Bin Laden, kana kwamba angehitajika kutoroka kwa haraka.

Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder amesema serikali hiyo inatarajia kuongeza majina mengine kwenye orodha ya magaidi wanaotakikana na Marekani, kufuatia habari walizopata katika nyumba ya Bin Laden.

Wakosoaji wameelezea wasiwasi wao kuhusu uhalali wa oparesheni hiyo, baada ya Marekani kubadilisha maelezo kuhusiana na kuuwawa wa Bin Laden akiwa ajajihami kwa silaha.


kwa hisani ya bbc swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.