ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 31, 2011

MTEMI MILAMBO FESTIVAL NI JULY 8-10 TABORA.

TAMASHA la ngoma za utamaduni na maonyesho ya biashara la Mtemi Milambo linatarajiwa kurindima kuanzia Julai 8 hadi 10 kwenye Uwanja wa Chipukizi mjini Tabora.Meneja wa Bia ya Balimi Bi.Edth Bebwa na Amon Mkoga Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam leo (30/05/2011), Mkurugenzi wa taasisi ya Chief Promotions ambao ndio waandaaji, Amon Mkoga, alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuenzi na kuuendeleza utamaduni wa Kitanzania, hususani makabila makubwa ya mikoa ya Tabora, Shinyanga na Mwanza, ambao ni Wanyamwezi na Wasukuma.

Mkoga alisema pia michezo na maonyesho ya bidhaa zenye asili ya Kitanzania pia vitakuwepo,kama vile mchezo wa bao na kurusha mishale. Alisema, Ijumaa ya Julai 8 shughuli itaanza saa 4:00 asubuhi hadi 12:00 jioni na kuendelea kwa muda huo huo hadi Jumapili Julai 10.


MTEMI MILAMBO pichani mnamo mwaka 1885-->

Mkurugenzi huyo alizitaja baadhi ya ngoma zitakazokuwemo wakati wa tamasha hilo kuwa ni pamoja na Manyanga, Maswezi, Uyeye, Bagalu, Bagika, Bazuba, Radu na nyinginezo.
Naye Meneja wa Bia ya Balimi, ambao ni kati ya wadhamini wa tamasha hilo,Bi Edith Bebwa, alisema wameamua kujitosa kudhamini tamasha hilo kwa mara ya pili ili kuwaenzi wateja wa bia hiyo ambayo ni mahususi kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa. “Ngoma hizi za Wasukuma na Wanyamwezi huchezwa sana wakati wa mavuno, hivyo kwa kuwa Balimi ni bia ya mkulima tumeona tuungane kusherehea pamoja wakati wa mavuno huku tukienzi utamaduni wa Kitanzania,” alisema Bebwa.

Mgeni rasmi katika Tamasha hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Abeid Mwinyimusa.

Kauli mbiu ya Tamasha hili mwaka huu ni KUSHOKE KUKAYA yaani turudi nyumbani tafsiri ya Kiswahili toka kinyamwezi.

Mbali ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi, wadhamini wengine ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ubalozi wa Switzerland ,Kalunde General Supplies, UNESCO na Fly 540(Shirika la ndege),Geita Goldmines, Magic Fm, Channel Ten na TBC.


Aksanteni kwa kunisikiliza na karibuni Tabora

Amon Mkunga
Mkurugenzi Mtendaji
Chief Promotions
P.O.Box 78566
Simu: 0755 638 004/0655 638 004
Barua Pepe:dramontz2002@yahoo.com
Tovuti:www.chiefpromotions.or.tz
Dar es Salaam
Tanzania

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.