ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 30, 2011

WATANZANIA LEO KAZI NI MOJA TU!

Leo kazi ni moja tu. Kila Mtanzania atakayekwenda Uwanja wa Taifa, anataka kuona Waganda, The Cobs wakitoka uwanjani vichwa chini kama ilivyokuwa Cameroon, katika mchezo wa marudiano wa kuwania kucheza Michezo ya Afrika itakayofanyika baadaye Septemba, Maputo Msumbiji.

Mchezaji wa timu ya Vijana ya Manyara Stars Mbwana Samata (kushoto) akimpiga chenga Idrisa Abdulahim, kwenye mazoezi.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Kampala, Uganda ilishinda mabao 2-1, hivyo vijana wa Tanzania leo wanahitaji ushindi wa bao 1-0 waweze kusonga mbele.

Kocha wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo 'Julio' alisema jana kuwa hana cha zaidi ya kuona timu hiyo inafanya vizuri katika mchezo huo. "Unajua mimi kawaida yangu namalizia nyumbani wao wanatambia kwao na mimi nikija kwangu natamba, sasa bora aliyeanza kwake," alisema Kihwelo.

Kihwelu alisisitiza kuwa kikosi chake kiko fiti kisaikolojia na kila mchezaji amejiandaa kwa ushindi na zaidi aliwaomba mashabiki kuishangilia kwa nguvu timu hiyo kama ilivyokuwa mchezo wake na Cameroon kuwania kucheza Michezo ya Olimpiki mwakani jijini London.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.