ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 11, 2011

UZINDUZI WA ALBAMU YA MIRIAMU LUKINDO ‘NI ASUBUHI’ WAFANA DIAMOND JUBILEE…!!!

Ni katika ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar es salaam ndani ya siku njema ya jana jumapili ndipo shughuli ya uzinduzi huu wa album ilipofanyika.Mwanamuziki wa nyimbo za injili Miriam Lukindo akiimba wimbo wa Ni Asubuhi wakati wa uzinduzi wa albamu yake ya nyimbo za injili inayokwenda kwa jina hilo hilo ‘Ni Asubuhi'.

Miriamu Lukindo (kushoto) akicheza sambamba na waimbaji wake katika uzinduzi wa albamu yake ya nyimbo za Injili jana jioni.

Vijana machachari katika uimbaji wa nyimbo za injili wanaojulikana kwa jina la ‘The Voice’ wakitumbuiza jioni ya leo katika ukumbi wa Diomond Jubilee katika kusindikiza uzinduzi wa albamu ya Miriamu Lukindo.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jordan Rukimbana (kushoto) akipokea CD ya nyimbo za injili kutoka kwa Miriam Lukindo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa albamu hiyo. Rugimbana ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu hiyo ya Miriam Lukindo inayokwenda kwa jina la ‘Ni Asubuhi’ katika ukumbi wa Diomond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa hisani ya www.mjengwa.blogspot.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.