ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 27, 2011

'UWASHAJI MOTO KWA KUTUMIA BIDHAA ZA PLASTIKI UNAZALISHA SUMU HATARI KWA BINADAMU' MKUTANO WA MAZINGIRA WABAINISHA.

Ni mkutano wa siku mbili uliolenga kuainisha mkataba wa Stockholm kuhusu kemikali zinazochukua muda mrefu kutoweka katika mazingira jinsi zilivyo na madhara kwa binadamu hasa zichomwapo sambamba na kujipanga kuwafikia wananchi kuwapatia elimu tosha kwa lengo la kulinda afya zao.Katibu tawala mkoa wa Mwanza Bi. Dorothy Mwanyika akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa mazingira uliofanyika Lakairo Hotel Mwanza, Pichani kushoto ni Profesa Jamidu katima, mhadhiri toka chuo kikuu cha Dar es salaam na kulia kwake ni Tutubi Mangazeni ambaye ni mkurugenzi wa utawala na raslimali watu ofisi ya makamu wa rais.
Bi. Mwanyika ameiasa jamii kuepuka vitendo vyote vinavyochangia kwa kasi uzalishwaji wa kemikali hizo zenye madhara kwa binadamu ambazo husababisha maradhi kama saratani katika maeneo mbalimbali mwilini mabadiliko katika mfumo wa kinga na madhara katika mfumo wa fahamu.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof Jamidu Katima.
Polychlorinated dibenzo-p-dioxins (PCDD) kwa kifupi dioxin na polychrinated dibenzofurans (PCDF) kwa kifupi furans ni kemikali mbili miongoni mwa kemikali 12 zinazochukua muda mrefu kutoweka katika mazingira ambazo zinathibitiwa kwa lengo la kulinda afya ya binadamu.

Zaidi na zaidi mkutanoni.
Kemikali hizi huzalishwa bila kukusudia wakati wa mchakato wa shughuli za uzalishaji bidhaa viwandani na uchomaji taka. Shughuli nyingine ambazo zimetajwa kama sehemu ya uzalishaji sumu hatari kwa afya ya binadamu ni pamoja na uchomaji taka za hospitali kwa kutumia mitambo isiyo bora, uzalishaji wa bati na chuma, uzalishaji wa saruji, chokaa, matofali na vioo, mitambo ya kuzalisha nishati inayotumia mafuta, kuni au mabaki mengine ya wanyama na mimea.

Mratibu wa warsha Bi. Magdalena John.
Kwa upande wake ameiasa Jamii kuepuka kuchoma taka ngumu hata zile zenye dutu za sumu au kuwasha jiko la mkaa kwa kutumia bidhaa za plastiki na kwa wale wenye viwanda amewataka kujiunga na teknolijia bora zilizopo za utunzaji mazingira kwa kuzingatia miongozo iliyoandaliwa na Sekretarieti ya mkataba wa Stokholm ambapo serikali imedhamiria kuifikisha kwa kila kiwanda.

Wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Mwanza katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili kujadili kuhusu mazingira kufanyika.

Utunzaji mazingira si kwa kupanda miti pekee bali wahusisha hata hewa mwanadamu aivutayo ambayo ni muhimu zaidi.

Mipango kudhibiti imeundwa kubaini na kudhibiti uzalishaji wa kemikali hatarishi kwa mazingira kwa kutoa elimu ya madhara ya sumu hiyo hatari sambamba na kukuza upatikanaji wa njia mbadala wa kuzuia uteketezaji wa taka ngumu.

kwa msaada zaidi angalia tovuti www.pops.int

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.