ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 23, 2011

TAMASHA LA PASAKA LASUBIRIWA KWA HAMU KUHITIMISHWA MWANZA JUMANNE YA PASAKA

MWENYEKITI wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha kubwa la Pasaka, Alex Msama amesema kwamba maandalizi yote yamekamilika na ikiwa sambamba na waimbaji kutoka nchi mbalimbali kuwasilini nchini.Msama ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Msama Promotions, amesema kwamba wanamuziki hao tayari wamekwisha wasili nchini kwa ajili ya tamasha hilo ambalo la kwanza litafanyika siku ya sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo baada ya kufanyika jijini Dar es Salaam pia litafanyika mjini Dododma Aprili 25 na baadaye Mwanza Aprili 26 na wakati huo huo, kwaya ya Kinondoni Revival Choir imethibitisha kushiriki kwenye Tamasha hilo la Pasaka ikunganana na waimbaji wengine.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu linawashikisha waambiji wote nyota wa muziki wa Injili wanaotamba nchini na pia wengine kutoka nyingine barani Afrika. Waaimbaji watakaoshiriki kwenye Tamasha hilo ni pamoja na Rose Mhando, Boniface Mwaitege, Christina Shusho, Updeno Nkone, Faraja Ntatoba kutoka nchini DR Congo, Ephraime sekeleti kutoka Zambia na Anastazia Mukabwa kutoka Kenya.
Wengine ni Solomon Mukubwa, Geraldine Odour na Pamela Wandela wote kutoka nchini Kenya.


Pia katika kilele cha Tamasha hilo ndani ya jiji la Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Aprili 26 mwaka huu ambayo itakuwa Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar itazinduliwa albamu mpya ya muziki wa Injili ya Haleluya Collections Vol 5. Albamu hiyo imeandaliwa na kusambazwa na Msama Promotions na malengo yake ni kusaidia watoto yatima na misaada kwa wanawake wajane.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.