ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 7, 2011

MATEMBEZI YA KUMUENZI RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR YAFANYIKA LEO. NAMI NA UJUMBE''''

Picha na Ramadhan Othman Abdalla.
Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya taifa CCM,Dk Ali Mohamed Shein,akipokea matembezi ya kumbu kumbu ya miaka 39 ya kumuenzi muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar,hayati Abeid Amani Karume,katika viwanja vya CCM Afisi kuu Kisiwandui leo.

Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya taifa CCM,Dk Ali Mohamed Shein huku wakionesha bango lenye Picha na ujumbe wa kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar,wakati wa mapokezi ya matembezi ya kumuenzi rais huyo yaliyopokele wa na Rais wa Zanzibar katika viwanja vya CCM Afisi kuu Kisiwandui leo.

Leo tunapoadhimisha kumbukumbu ya mapinduzi ya zanzibar ya tarehe 12 january 1964 kuna haja kuikumbusha serikali kuwa kuna jambo moja muhimu inalopaswa kulizingatia katika kutunza kumbukumbu na kukilinda kizazi chake nalo ni Kuweka utaratibu utakaowawezesha vijana wake wa sasa kupata elimu ya kujua historia ya matukio muhimu ya taifa letu la Tanzania. Kwani ndani ya zama hizi kumekuwa na mkanganyiko katika masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa kutokana na kizazi cha sasa kuuweka kando 'wakati uliopita' na kuzingatia 'wakati uliopo' na 'wakati ujao'.

KARUME DAY OYEEE
@g.sengo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.