ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 29, 2011

KATIKA KUELEKEA KILI TAIFA CUP TBL WACHANGIA MAANDALIZI YA MWANZA HEROUS.

Meneja wa mauzo wa kampuni ya bia Tanzania TBL tawi la Mwanza bw. Maliki Sitaki akikabidhi fedha taslimu shilingi milioni 1.5 kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Abass Kandoro kama sehemu ya mchango wa kampuni yake kusaidia maandalizi ya awali kwa timu ya mkoa wa Mwanza (Mwanza Herous) itakayoshiriki michuano ya ligi ya Taifa inayotaraji kuanza kutimua vumbi may 7/2011.

Meneja wa mauzo na usambazaji TBL kanda ya ziwa Malaki Sitaki (aliyesimama), pembeni yake ni Special Event Manager wa kampuni hiyo Erick Mwayela na mwisho kabisa ni Katibu tawala mkoa wa Mwanza Bi. Dorothy Mwanyika. Jumla ya timu 23 za mikoa mbalimbali hapa nchini zimepangwa kushiriki michuano ya Kili Taifa Cup 2011 kwa makundi sita ambapo kila mkoa umetengewa fungu lake kwa ajili ya maandalizi ya awali.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mchango huo na kisha kuuwasilisha papo hapo kwa mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mwanza (MZFA) Jackson Songora, mkuu wa mkoa wa Mwanza Abass Kandoro amesema ofisi yake itatoa shilingi milioni moja kuchangia maandalizi hayo ambapo mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 3.8 zinahitajika kwenye bajeti ya shilingi milioni 7 iliyowekwa.

Pia mkuu huyo ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo, mashirika binafsi na wafanyabiashara wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kuisaidia timu hiyo ili ishiriki vyema kwenye mashindano hayo na hatimaye ipate ushindi.

Awali mashindano hayo soka ya Taifa Cup ndani ya TBL yalikuwa yakidhaminiwa na bia ya Safari Lager ambapo kampuni hiyo baadae katika maamuzi yake na sababu maalum iliamua kuhamisha udhamini wa michuano hiyo kwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.