ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 29, 2011

PRINCE WILLIAM NA KATE SASA NI WANA NDOA KAMILI

Tabasamu la ukweli limetawala kwa wapenzi wawili Prince William na Kate Middleton mara baada ya ndoa yao takatifu kufungwa katika kanisa la Westminster Abbey, mjini London ikiwa ni mbele ya mashuhuda waalikwa wapatao 1,900 na watu takribani bilioni 2 walioshuhudia tukio hilo sehemu mbalimbali duniani kupitia luninga zao.

Maharusi hao walishangiliwa na maelfu ya watu waliojipanga barabarani kuelekea kasri ya Buckingham Palace ambako Malkia amewaandalia karamu wageni 650.


Mwana mfalme William akifungishwa ndoa na Aksofu Rowan William katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.

Wana ndoa hao wapya walitumia gari liliovutwa na farasi la muundo wa mwaka 1902 ambalo lilitumiwa na wazazi wake Prince William wakati wa ndoa yao mwaka 1981 ambapo baadae maharusi hao walijitokeza kwenye roshani ya kasri ya Buckingham na kuwasalimu maelfu ya watu waliokwenda kuwasherehekea.

Si wawili tena bali ni mwili mmoja.
Baada ya kulishana viapo vya ndoa Askofu mkuu wa Canterbury, Rowan Williams, aliwanadi rasmi kuwa "mume na mke". Kuanzia sasa maharusi hawa watajulikana rasmi kama Duke na Duchess wa Cambridge.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.