ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 7, 2011

UNITED YAANGUKIA PUA, TENA

Liverpool jana imeichapa Manchester United kwa mabao 3-1, katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Anfiled.Dirk Kuyt alifunga mabao yote hayo matatu katika mchezo uliotwaliwa zaidi na Liverpool. Mabao yalifungwa katika dakika za 34, 39, na 65. Bao pekee na la kufutia machozi lilifungwa na Havier Hernandez katika dakika ya 90.

Mkali wa Liverpool ambaye bado hajaimarika vizuri kutokana na majeraha yanayo mkabiri Andy carroll (c)akichuana na beki mahiri wa man u, mfaransa Patrice Evra.

Wachezaji wa pande zote mbili katika malumbano baada ya mlinzi wa mashetani wekundu mbrazili Rafael Da Silva's kumchezea faulo mchezaji wa Liverpool ambaye pia ni mbrazili Lucas Leiva.

Mchezaji wa Manchester United Nani akiondoshwa kwa machela dimbani hapo mara baada ya kuumia kupitia kuchezewa vibaya na Jamie Carragher.

Liverpool's Dutch forward Dirk Kuyt (L) akisherehekea baada ya kutupia goli la tatu katika mchezo huo. United wanasalia kileleni wakiwa na pointi 60, huku Liverpool wakiisogelea Tottenham kwa kufikisha pointi 42, huku Spurs wakiwa na 47.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.