ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 31, 2011

MBUNGE WA CHADEMA ILEMELA MWANZA ATIMIZA AHADI YAKE NDANI YA SIKU 90 ZA UONGOZI WAKE. MH. SUGU ALAZIMISHWA KUCHANA SHANGWE ZALIPUKA!!!

MBUNGE wa Jimbo la Ilemela, mkoani hapa, Mh. Highness Samson Kiwia, amewataka wananchi kutunza vitendea kazi mbalimbali vinavyotolewa na wafadhiri, serikali na taasisi mbali mbali ili viweze kutumika kwa muda mrefu kwa manufaa yao.MH. MBUNGE (KULIA) AKIKABIDHI MSAADA HUO.
Alisema hayo wakati alipokuwa akikabidhi gari la kubebea wagonjwa aina ya Nissan Patrol lenye thamani ya shs.millioni 32 katika hafla fupi iliyofanyika katika Zahanati ya Karume, iliyopo katika kata ya Bugogwa wilayani Ilemela.

Katika kampeni za uchaguzi ambao ulimalizika mwishoni mwaka jana, aliwahaidi wananchi katika jimbo lake kuwa atawasaidia gari la kubeba wagonjwa ambalo litawasaidia wananchi kuwasafirisha hadi katika hospitali zingine na baadhi yao kuwatoa majumbani kwao hadi katika zahanati hiyo ahadi ambayo ameitekeleza ndani ya siku 90 kama alivyoahidi.

WANANCHI WAKITATHMINI GARI LAO.
Mhe.Kiwia ametoa ahadi nyingine kuwajengea wananchi wa kata ya Bugogwa, kituo cha polisi na kumuagiza Diwani wa Kata ya Bugogwa, Swila Dede Swila ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo, kata ya Bugogwa kusimamia ujenzi wa kituo hicho ambacho kitaanza kujengwa muda wowote kuanzia sasa na ujenzi wake kukamilika ndani ya siku 90.

Mganga Mfawidhi katika Zahanati ya Karume, Bernard Straton, amemshukuru mbunge kwa msaada huo na kuongeza kuwa gari hilo ni msaada mkubwa kwa wananchi wa kata ya Bugogwa na kumuomba mbunge huyo kutoa ufadhiri wa aina nyingine pale ambapo utahitajika katika zahanati hiyo.

MH. AKICHANA' MISTARI.
Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi al maarufu kwa jina la Mr. sugu alikabiliwa na wakati mgumu baada ya kulazimishwa kuimba jukwaani pasipo kupanga, hiyo ni mara baada ya kuhutubia. "Tunataka UCHANE" , "CHANA MISTARI NDIYO UKAE" sauti zilisikika! Bila hiyana akawapa mistari ya kutosha ya wimbo - Wananiita sugu! ......Akashangiliwa ile mbaya na mamia yaliyohudhuria makabidhiano hayo.

Ametoa maelekezo kwa watendaji ngazi ya kata kuwa na ushirikiano wa karibu katika kukamilisha mipango mbalimbali aliyoiweka ikiwa ni pamoja na ujenzi huo wa kituo cha polisi, kufanya kazi bila kutegeana na kusema kuwa suala la ulinzi ni haki ya kila mwananchi na hivyo kukamilika kwa kituo hicho itakuwa ni mojawapo ya kuwahakikishia usalama wao na mali zao.

MBUNGE HIGHNESS AKITIA SAINI KITABU CHA MAKABIDHIANO.
Mbali na hayo, mh. Mbunge pia ameahidi kuendeleza miradi mingine ikiwemo ukarabati wa barabara, usambazaji wa maji safi kuwa itasimamiwa kikamilifu lengo likiwa ni kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata ya Bugogwa na jimbo la Ilemela kwa ujumla.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.