ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 22, 2011

KUNDI LA MUZIKI WA TAARAB FIVE STARS LAPATA AJALI MBAYA WANAMUZIKI 13 WAFARIKI DUNIA.

Ajali mbaya ya gari imetokea jana usiku katika Mya Mikumi. Ajali hiyo imehusisha gari aina ya coaster lililokuwa limewabeba wanamuziki wa bendi ya muziki wa Taarab ya Five Star Morden Taarab na kusababisha vifo vya wanamuziki 13 wa kundi hilo akiwemo muimbaji maarufu wa kiume Issa Kijoti.

Marehemu Issa Kijoti enzi za uhai wake.

Gari hilo lilikuwa na jumla ya watu 22. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari mbalimbali inadaiwa kuwa gari hilo lilikuwa kwenye mwendo mkali likijaribu kuovateki na hatimaye kugonga roli lililokuwa limepakia mbao pembeni mwa barabara. Miili imeheribika vibaya sana kiasi cha kusababisha zoezi la utambuzi kuwa gumu.

Mwanahawa Ally yu mmoja kati ya wanusurika wa ajali hiyo aliye ambatana na kundi hilo kama msanii mwalikwa wakitokea mjini Songea ambako walikuwa kwenye ziara yao ya kimuziki na walifanya onyesho lao juzi hivyo jana wakawa wakirejea jijini Dar. Anasimulia kuwa kwa bahati mbaya walipofika maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro basi lao likapata ajali, naye akijeruhiwa mkono na kupata majereha kadhaa kichwani na sehemu nyingine za mwili.

Taarifa zaidi tutaendelea kukupatia kadri zinavyotufikia,
Pole 5stars Morden Taarab Pole Tanzania.
@ALBERT G. SENGO.

Tupe maoni yako

2 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.