ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 2, 2011

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AVUMISHIWA KIFO. BABA + MKUU WA WILAYA WAKANUSHA WASEMA YU HAI.

Siku ya jana hapa nchini zilizagaa Tetesi za kifo cha brigedia mstaafu dr Yohana Balele, vyombo vingi vya habari viliripoti juu ya taarifa hizo huku mitandao nayo ikitoa usaidizi wa kutosha kupenyeza kwa kasi ya ajabu taarifa hizo za majonzi.
Kupitia uvumi huo familia ya brigedia huyo mstaafu ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga siku nzima ya jana ilipata usumbufu kwa kupokea simu nyingi si kutoka kwa watu wa hapa nchini pekee bali hata watu kutoka mataifa ya mbali wakitaka kujua ukweli haswa na wengine kudiriki hata kutoa salamu za rambirambi kwa familia hiyo.

Taarifa za awali zilimtaja mkuu huyo kulazwa katika hospitali ya rufaa ya bugando ambako asubuhi ya leo blogu yako (gsengo) ilikwenda kuthibitisha ukweli na haikumkuta mkuu huyo. Lakini mara baada ya kufika hospitalini hapo mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe akapenyeza taarifa kuwa mkuu huyo wiki takribani tatu zilizopita aliletwa hospitalini hapo kupatiwa matibabu ambapo alilazwa kwa siku mbili tu! na baadaye kuhamia nyumbani kwa mkewe Isamilo jijini Mwanza huko aliendelea kupatiwa matibabu.

NYUMBANI KWA MKE WA DR. BALELE, ISAMILO MWANZA.
Simon Mtemi Majola ambaye ni baba wa mkuu huyo wa mkoa ni moja kati ya watu niliowakuta nyumbani kwa mheshimiwa maeneo ya Isamilo, ambapo Mzee Majola amekanusha taarifa hizo za kifo na kusema kuwa Dr Yohana Balele yu hai akiendelea na matibabu nyumbani hapo ila kwa wakati huo siwezi kuonana nae kwani amepumzika chumbani kwake.

Nae kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi.Amina Masenza ambaye vilevile ni mkuu wa Wilaya ya shinyanga Mjini akiongea na Clouds fm amekanusha Uvumi huo. Ndugu wengi kutoka vijiji vya mbali na mikoa ya jirani wamefika nyumbani hapo mara baada ya kupata taarifa hizo za uvumi.

WAKATI HUO HUO chanzo cha 'UVUMI' huu unatajwa na vyanzo visivyo rasmi kuwa:- Umetokana na moja ya mikutano wa chadema kwenye vijiji vya mkoa wa Shinyanga ambapo Dr. Silaa alipokea ujumbe kutoka kwa mtu ambaye hakutajwa, ujumbe ukimtaja mkuu wa mkoa wa shinyanga Dr. Balele kufariki dunia hali iliyomlazimu kuvunja mkutano.

Blogu hii inamtakia matibabu mema na afya njema mkuu wa mkoa wa shinyanga Dr. Yohana Balele.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.