ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 11, 2010

MKUTANO MKUU WA VIJANA VYUO VYA ELIMU YA JUU MWANZA WASHINIKIZA KUANZISHWA KWA BENKI YA VIJANA.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo mh. Emmanuel Nchimbi akihutubia ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, ambapo katika sehemu ya hotuba yake amewataka vijana kujiandaa kikamilifu kwa majukumu yaliyo mbele yao kwani Idara nyingi za serikali na Mashirika binafsi viongozi na watendaji ni vijana.

Waziri Nchimbi akifungua mkutano huo kwa ishara ya kukata utepe.

Waziri Nchimbi akitambulisha Cheti cha Ufunguzi. "Nitafarijika sana Ikiwa wasomi wengi watajihusisha na kuwekeza katika kilimo cha kisasa na ufugaji" Sehemu ya hotuba.

Mkutano huu ni matokeo ya maazimio ya mkutano uliofanyika Dodoma Mwezi juni ambapo uliazimia kufanyika kwa mikutano kama hii ya vijana katika kila kanda ili kujadili changamoto mbalimbali za kimaendeleo.

MA-FOUNDER WA TAYODEFO Kutoka kushoto ni Emmanuel Mgenge, Mgunda Bwere, Patrick Bryoba, Tumaini Kimaro na Christina Benard.

Wataalam wa maendeleo wanaamini kuwa elimu na fedha ni rasilimali muhimu kwa maendeleo hivyo mkutano uliopita wa Dodoma uliazimia pia Uanzishaji wa Benki ya Vijana.

Waziri nchimbi akiagana na wanavyuo mara baada ya kumwakilisha waziri mkuu (Mizengo Pinda) kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa vijana vyuo vya elimu ya juu uliofanyika katika ukumbi wa BOT CAPRIPOINT, MWANZA.

Kutoka kushoto: Mdau wa TAYODEFO, Mh.NCHIMBI na G.SENGO.

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na Ma-FOUNDER wa TAYODEFO. Vyuo vilivyoshiriki ni pamoja na Chuo kikuu cha mtakatifu Agustin (SAUTI), Chuo kikuu kishiriki cha Afya Bugando (BUCHS) na Chuo cha Elimu ya biashara (CBE) kampasi ya Mwanza. Mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya vijana kupigana vita juu ya UKIMWI na Madawa ya kulevya nayo ndani.

Friday, December 10, 2010

TANZANIA HIYOOOOO....FAINALI.

DAKIKA HII HII ....KIPA NAMBA MOJA JUMA KASEJA KAIBUKA SHUJAA BAADA YA KUOKOA MKWAJU MMOJA WA PENATI KATI YA MITANO, NI PENATI ILIYOPIGWA NAYE TONNY MAWEGE NA KUIWEZESHA KILIMANJARO STARS KUSHINDA KWA BAO 5-4 NI KATIKA MICHUANO YA TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP HATUA YA NUSU FAINALI.


KWA UPANDE WA KILIMANJARO STARS MAGOLI YA PENATI YALITUMBUKIZWA KAMA IFUATAVYO:-

1. NSAJIGWA
2. STEPHANO MWASIKA
3. SHAHBAN NDITI
4. MACHAKU
5. ERASTO NYONI


STARS KUKIPUTA FAINALI DHIDI YA IVORY COAST SIKU YA JUMAPILI.

KITABU CHA JK CHAZINDULIWA IKULU.

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Wasifu wa Maisha yake, akishuhudiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete na Mwandishi wa kitabu hicho Profesa Julius Nyang'oro jana mchana Ikulu, Dar es salaam

Mwandishi wa Kitabu cha Wasifu wa JK Profesa Julius Nyang'oro akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua kitabu hicho ambacho alikiandika na kuelezea sababu mojawapo iliyomfanya aandike kitabu hicho ni kutokuwa na kitabu cha aina hiyo kwa viongozi wetu wa nchi isipokuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wakiongea na Profesa Nyang'oro ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha Wasifu wa JK wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Maendeleo ya Vijana Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Shukuru Kawambwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo akizungumza na Bi. Amina Mtengeti ambaye ni Shangazi wa Profesa Nyang'oro mwandishi wa kitabu cha JK wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. Pichani ni viongozi wengine wa kitaifa na marafiki wa Profesa Nyang'oro waliohudhuria uzinduzi huo.

Vitabu hivyo vimeanza kuuzwa kwenye duka la vitabu la Chuo Kikuu Cha Dar es salaam rasmi kuanzia leo tarehe 10-12-2010 kwa gharama ya shillingi 25,000/=


PICHA KWA HISANI YA IKULU.

FBME YATOA MSAADA KWA HOSPITALI YA SEKOU TOURE.

Katika kukabiliana na uhaba wa vitendea kazi na nyenzo kwa hospitali zetu nchini benki ya FBME kupitia tawi lake la Mwanza leo imekabidhi msaada wa mashuka na foronya 400 kwa hospitali ya mkoa wa Mwanza (SEKOU TOURE).
Meneja wa benki ya FBME tawi la Mwanza Joseph Gwalugano akikabidhi msaada huo kwa mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dr. Meshark Mmasi.

“Msaada huu ni sehemu ya mikakati ya FBME tuliyojipangia, kwa sababu tupo karibu na jamii na tunapaswa kujitolea kwa ari na mali katika kuhakikisha kuwa jamii inanufaika na misaada " Kauli ya Joseph Gwalugano ambaye katika picha hii anaonekana kulia kabisa akikabidhi msaada huo kwa mganga mkuu wa hospitali ya Sekou toure Dr. Onesmo Kimbera.

Wadau wa FBME wakishiriki zoezi la kutandika shuka hizo kwenye vitanda wodi ya akinamama wajawazito na watoto hospitalini hapo.

Ni maelezo toka kwa muuguzi juu ya jinsi shuka hizo zitakavyotumika kwenye wodi ya watoto waliokumbwa na majanga ya moto.

HAPA ni ndani ya jengo jingine lililo jipya kabisa la wodi ya watoto hospitalini hapo, Jengo limekamilika likisubiri vifaa na ufunguzi kisha lianze kazi.

Shukrani kwa benki ya FBME mwanza.

VIJANA NA MAENDELEO.

SHUGHULI NI KESHO (JUMAMOSI) NA KESHO KUTWA (JUMAPILI) PALE B.O.T CAPRIPOINT MWANZA, WASHIRIKI WAKIWA NI WANAFUNZI WAWAKILISHI WA VYUO MBALIMBALI.

WADAU JIPANGENI VYEMA.

Thursday, December 9, 2010

HAPPY INDEPENDENCE DAY!

LEO ni siku ya Uhuru wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika. Watanzania wote wanaadhimisha uhuru wa Tanganyika kutimiza miaka 49 tangu wakoloni wa Uingereza walipokabidhi hatamu za uongozi wa taifa hilo, ambalo sasa linajulikana kama Tanzania Bara, kwa wananchi wenyewe, Desemba 9, 1961. Maadhimisho ya siku hiyo yanawapa nafasi na changamoto kubwa Watanzania za kutafakari walikotoka, walipo na wanakokwenda li kuona wapi walikosea, kuteleza au kufanya vizuri, na kupanga mikakati ya kuondoa kasoro na kuweka mipango madhubuti zaidi ya kuendelea kulijenga taifa lao.
TATIZO LA MAJI SAFI NA SALAMA.
Yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali na wananchi tangu uhuru. Lakini pamoja na maendeleo hayo, zipo changamoto kubwa zilizokwaza harakati hizo za maendeleo, ambazo wakati wa kusherehekea miaka 49 ya uhuru, tunapaswa kuzitafakari na kuzipatia ufumbuzi utakaolipeleka mbele zaidi taifa letu.

MIAKA 49 YA UHURU WA TZ OYEEE..
NINA AMINI KUWA TUTAFIKA.

IMBAA...WIMBO WA DITTO - ZAMANI

VERSE 1...Siwezi Kuishi Bila Upendo wako Ulivyoniteka

Naomba Nihifadhi Kwa Mikono Yako Nisije anguka

Nimezunguka Kutwa Nzima Kama wewe sijamuona

Napigwa Vita Chungu Nzima Lakini Bado Napigana

CHORUS...Wapo walotaka Nikuache Nakusema Sitofika Popote

Ndipo Wakanifanya Niongeze Juhudi Nyingi mpaka siku Niwe wako

Sijali Umenitesa Mara ngapi Ama Nimelia Mara Ngapi

Nia Yangu Ni Moja Siku Moja Tuwe wote Pamoja x2

VERSE 2...Sijasahau Usiku Wa Manane ule Ulivyo Nikana

Mbele Ya Nduguzo Na Bwanaako Yule Ukanitukana

Kwa Mapenzi Nilisimama Kama Chizi Nilionekana

Leo Wakusema Hakuna Najua Waamini Nakupenda

CHORUS... Wapo walotaka Nikuache Nakusema Sitofika Popote

Ndipo Wakanifanya Niongeze Juhudi Nyingi mpaka siku Niwe wako

Sijali Umenitesa Mara ngapi Ama Nimelia Mara Ngapi

Nia Yangu Ni Moja Siku Moja Tuwe wote Pamoja x2

BRIDGE... Penzi Letu Liende mbele lisifike Mwisho oooooo

Tuwe Wote Milele Tushinde Vikwazo oooooo

Wapooooo Ooo oooo oo Wapooooooooooo

Wapoooooooo Wapooooooooooooooo

HOOK ... Sijali Umenitesa Mara Ngapi Ama Nimelia Mara Ngapi

Nia Yangu Ni Moja Siku Moja Tuwe Pamoja Haaaaaa x2

SUSTAINET WAZINDUA VITABU VYA MBINU ZA KILIMO ENDELEVU.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mh. Serenge Mrenge akizindua vitabu vya mbinu sahihi za kilimo vya shirika lisilo la kiserikali la SUSTAINET hii ni mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwaka wa shirika hilo, uliofanyika Lakairo hotel Kirumba jijini Mwanza, nchini Tanzania. Katikati ni katibu mkuu mtendaji wa mradi huo Tom Apina akifuatilia tukio hilo kwa umakini.

VITABU VYA ELIMU JUU YA MBINU SAHIHI ZA KILIMO.
Mradi wa SUSTAINET umefanikiwa kujumuishwa kama sehemu ya mtandao wa UN kupitia shirika lake la chakula na kilimo - FAO umejikita zaidi katika kutoa elimu kwa wakulima wadogo na kushirikiana nao katika kuwaelekeza mbinu sahihi za kuanzisha miradi waweze kujikwamua kutoka katika lindi la umaskini kupitia kilimo chenye manufaa (kilimo cha biashara).

Katika mkutano huo wa mwaka Mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa na hatimaye maazimio ya mkutano yakawa ni pamoja na shirika hilo kujipanua zaidi kuhakikisha kuwa kila mkulima ananufaika na elimu wanayoitoa.

Mh. Serenge akikabidhiwa seti nzima ya vitabu vya KILIMO toka kwa Edith Omamo ambaye ni mratibu wa Mradi huo wa shirika lisilo la kiserikali la SUSTAINET unaodhaminiwa na watu wa Ujerumani wenye mtandao wa kiushirika kwa vikundi vya watu binafsi kwa nchi za afrika mashariki za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela akiangusha sahihi kwenye moja ya vitabu vya kilimo vilivyozinduliwa.

BOARD MEMBER NA MKUU WA WILAYA.
Traditional practices can be improved and combined with alternative ecological forms of land use, resulting in comprehensive systems for sustainable agriculture. A wealth of experience drawn from every continent confirms that these approaches have great potential, which is still significantly under-exploited. But before these successful approaches can be disseminated on a massive scale, numerous obstacles have to be overcome. Generally the potential users of sustainable agriculture do not have enough access to the information they need. An equally common problem is that political, social and economic structures in a country can inhibit the implementation of such approaches. Under the auspices of its National Strategy for Sustainable Development, the German federal government supports the SUSTAINET project, which aims to overcome these obstacles.

Wednesday, December 8, 2010

KARIBU TENA...

MV VICTORIA: SAFARI ZAKE MWANZA TO KAGERA.
Mwezi wa mapumziko ya mwaka ndiyo huu na ndicho kipindi tunachokwenda kubadili kalenda marafiki kutoka mikoa ya mbali karibuni na kwa wale wanaokwenda sehemu na sehemu basi blogu hii yawatakia kila la kheri na kama vipi tutumiane hizo photo iwe zenu, za mazingira, matukio kupitia email:

albertgsengo@yahoo.com


HAZINA ZA JIJI LA MWANZA KWA UTALII.
Picha hii niliipiga last weekend nikiwa kwenye mtumbwi wakati navua samaki kwaajili ya kitoweo.

MALAIKA BEACH HOTEL.
Mkutano wa uwekezaji Bonde la ziwa Victoria uliomalizika leo Ulifanyika hapa na wageni kulala hapa. Hoteli iko karibu na Tunza beach...on the way to the airport you branch off on your left (around Ilemela)..then follow road signs...dust road though.
SWIMMING POOL JUU YA MAJI.
Rafiki yangu Magonda anasema, "Mwaka huu nitakuwa na likizo na nilikuwa nimepanga kwenda kupumzika kijijini. Kabla ya kufika kijijini, ni lazima upitie Mwanza. Nimeshapata mahali pa kupumzika, ahsante kwa habari..."

Ka mtumbwi kangu kaleeeeee! nimesahau kutia nanga kameenda na upepo.

Je! unaona nini katika hii picha?

Tuesday, December 7, 2010

SHANGAA SHANGAA BASI MATUKIO NA MAZINGIRA!!

IMEDIZAINIWA TU WADAUUUU..... WACHA NIITOEEE


AyyAaaaaaa!!! Duh! Kama boga vile limepitiwa na tairi la gari. Ngoma kama hii unaambiwa tafuta pua ya marehemu.

Mmmh ajali zingine..TEHE! TEHEee!!!

KhAAh! WE NAWE! sa ndo nini sasa!!!

Monday, December 6, 2010

HEPI BAZDEI 2 MY QUEEN.

MDAU WANGU WE MKAREE' SI unamjua yule shemeji yako wa karibu haswaaa na na si wa mbaree, ambaye anasababisha joto langu lisipotee na liwe pare-paree'LEO NI SIKU YAKE YA KUZALIWA.
MY WIFE WANGU NA MWANAE CATHBERT.

CEDRICK NA CATHBERT.

HAPPY BIRTHDAY OLIVA.SERVICE KWA WADAU.

KEKI KWA SECOND KID.

KWA DADA AKA WIFI.

NA MIE....PAREEE

KWAAaa SIS KULWA.

MKUTANO WA UWEKEZAJI BONDE LA ZIWA VICTORIA WAANZA JIJINI MWANZA.

Wananchi wanaozunguka eneo la Bonde la Ziwa Victoria wanaendelea kukabiliana na hali ngumu ya maisha na kuishi katika hali ya duni ya maisha, ingawa eneo hilo limejaliwa utajiri wa uoto wa asili na raslimali za kutosha.
MEZA KUU YA KUSANYIKO HILO.
Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Maji Prof. Mark Mwandosya wakati alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kusanyiko la kwanza la uwekezaji katika Bonde la Ziwa Victoria lililofanyika jijini Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wawekezaji kutoka katika nchi za Afrika Mashariki.

WAZIRI MWANDOSYA NA BALOZI MWAPACHU WAKIWASILI ENEO LATUKIO.

MH. MWANDOSYA.
Mwandosya amezitaja changamoto zinazochangia kuwepo kwa hali hiyo ni pamoja na umaskini, migogoro ya kiuchumi, ukosefu wa raslimali watu matumizi mabaya ya vyanzo vya maji , uchafuzi mazingira na ukuaji wa kasi ya ongezeko la watu.

HAFSA MOSSI.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Hafsa Mossi amesema kuwa kutokana na raslimali zilizo katika Bonde la Ziwa Victoria, ana imani kuwa wawekezaji wenye sifa watajitokeza kuja kuwekeza kwa lengo la kuwaondolea umaskini wakai wanaozunguka bonde hilo.
Amefafanua kuwa mbali na wananchi kunufaika na ajira, kutokana na uwekezaji huo watapata fursa ya kujipatia maendeleo kwa kujifunza mbinu bora za kisasa za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, vyanzo vya nishati ya umeme na usafirishaji na hivyo kuondokana na umaskini wa kipato.

Kusanyiko hilo la kwanza la uwekezaji katika bonde la Ziwa Victoria linalofanyika kwa siku tatu Malaika Hotel Mwanza ambapo jumatano ni hitimisho, Limefanyika likiwa na lengo la kubainisha faida za kiuchumi na kijamii zilizopo bonde la ziwa victoria na kuweza kuvutia wawekezaji kwenda kuwekeza.

WADAU wakijadili haya na yale mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

The Deputy Prime Minister for Uganda (who seated) posses in a group photo with other East African leaders at Malaika hotel grounds yesterday. From right who seated are the RC for Mara Region Enos Mfuru, The Secretary General for East African Community Ambassador Juma Mwapachu, The Minister for Water Prof Mark Mwandosya, The Deputy Prime Minister for Uganda Hon. Eriya Kategaya, The RC for Mwanza Abbas Kandoro and The Executive Secretary for THE Lake Victoria Basin Commission Dr. Tom Okurut.