ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 20, 2010

NYAMIZI'S KITCHEN PARTY!!

CHEREKO ZA KITCHEN PARTY NA SAFARI HII NI KWA NYAMIZI MOHAMED KASSANGA.

WOW!!

WAUKWELI.COM

USAFI JADI YETU MWANAKWETU...

MAPISHI JEH! SEKTA MUHIMU YA KUZALISHA ENERGY KWA FAMILIA.

DECORATION AKA MAPOUDAzz!

SHUGHULI ILIFANYIKA TAREHE 20/JUNE/2010 GADHI HALL MWANZA NA BAADAE HARUSI YA NGUVU. (PICHA ZA HARUSI ZAJA).

FLOWERS WALIPENDEZAJE!!

CHAKULA KITAAAAAM'

ZAWADI NI ZAWADI...!

ALITUNZWA HASWAAA...!!

MABIDADA NA MASHOSTI KIMPONGEZA BI HARUSI MTAJIWA.

Friday, November 19, 2010

MAADHIMISHO YA SIKU YA CHOO DUNIANI MKOANI MWANZA.

Mila potofu zimetajwa kuchangia kwa asilimia kubwa maambukizi ya maradhi yatokanayo na kukiuka kanuni za afya na usafi, likibainika katika utafiti uliofanywa kwa wakazi wa vijiji vya wilaya ya Magu, ambapo familia moja yenye zaidi ya watu kabla ya kula, hunawa maji kwenye bakuli moja kasha mara baada ya hapo mzee wa familia huyanywa maji hayo kama tiba ya kutanua kifua au humnywesha motto mchanga kwa makusudi hayo ya kumpanua kifua.

Takwimu za vyoo katika jiji la mwanza zinaonyesha kuwa vyoo bora ni asilimia 64%, vyoo duni ni asilimia 33% na nyumba ambazo hazina vyoo kabisa ni asilimia 3%, changamoto ya tatizo hilo ikitajwa kuwa ni pamoja na gharama kubwa ya vifaa vya ujenzi, umasikini na ufukara wa wananchi kutokana na kipato duni na kiwango cha uelewa,na hali ya miamba na baadhi ya maeneo kuwa na chemichemi nyingi hasa mabondeni.

Kwa upande wa matumizi ya vyoo kulingana na hali ya kijiografia na jinsi ujenzi holela milimani ulivyo, imegundulika kuwa siyo kwamba nyumba zote zilizoko sehemu za milima hazina vyoo bali taarifa sahihi ni kwamba vyoo vilivyopo maeneo hayo siyo bora na si vya kudumu.

Sambamba na maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa kila halmashauri nchini huku mkoa wa Tanga yakifanyika kitaifa , halmashauri ya jiji la Mwanza kwa kushirikiana na PLAN INTERNATIONAL imefanya maonesho katika viwanja vya furahisha ya choo rahisi bora na cha kisasa kama darasa kwa wananchi.

HEPI BARZDEY BRAZAz.

DJ MAHIRI WA CLOUDS FM NA BODA2BODA YA TBC ONE, DEEJAY ARON LEO ANAZALIWA.

UMEZALIWA TAREHE MOJA NA CALVIN KLEAN ALIYEZALIWA 19NOV1942 HUYU NI MBUNIFU MAARUFU WA MAVAZI NA MITINDO LEBO YAKE (CK) IKITHAMINIKA NA KUTAMBULIKA KONA NA KONA ULIMWENGUNI.



VILE VILE:-
LARY KING MFANYAMAHOJIANO MAHIRI WA TV NA RADIO, MTUNZI NA MHARIRI ANAYEKUBALIKA, ALIZALIWA TAREHE 19NOV1933.

HAPPY BIRTHDAY 2 YOU ALL.

Thursday, November 18, 2010

SONGI LA HIP HOP ALILOIMBA RAIS MU7 LAMTIA KIWEWE.

HII NI REMIX KATIKA STYLE YA KATUNI.

MKUU WA IDARA YA HABARI YA RAISI WA UGANDA YOWERI MUSEVENI AMESEMA KUWA SIFA YA RAISI HUYO IMEHARIBIWA VIBAYA KUTOKANA NA MZIKI WA RAP ALIOUIMBA MWEZI ULIOPITA.
TAMALE MIRUNDI AMESEMA WALAGHAI WAMEHARIBU PICHA ZA MUSEVENI, WAKITUMIA KOMPUTA, NA KUMFANANISHA NA NYOTA WA MUZIKI WA HIPO HOP ANAYEIMBA AKIWA NUSU UCHI.

BAADHI YA PICHA HIZO ZINAONYESHA AMEVALIA MKUFU SHINGONI HUKU AKIWA NA PICHA ALIZOCHORWA MWILINI MAARUFU KAMA ''TATTOOS''..

RAIS MUSEVENI ANAWANIA MUHULA MWINGINE KAMA RAIS WA UGANDA KUPITIA CHAMA CHA NATIONAL RESISTANCE MOVEMENT NRM.

NOTI BANDIA ZAKAMATWA MWANZA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MWANZA NONOSIUS KOMBA.

JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KOSA LA KUMILIKI NOTI BANDIA ZENYE THAMANI YA SHILINGI LAKI NANE NA SABINI ELFU.

AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KAIMU KAMANDA WA POLISI MWANZA NONOSIUS KOMBA AMEMTAJA MTUHUMIWA HUYO KUWA NI BW. SILAS OMOLO (29) MKAZI WA ENEO LA NYEGEZI WILAYA YA NYAMAGANA.

AMESEMA KUWA MNAMO TAREHE 16NOV2010, SAA TISA NA DAKIKA ISHIRINI JESHI HILO LILIFIKA ENEO LA TUKIO NYEGEZI JIJINI MWANZA NA MARA BAADA YA UPEKUZI MTUHUMIWA SILAS OMOLO ALIKUTWA NA NOTI 87 ZA SHILINGI ELFU KUMI, KUMI AMBAPO NOTI 30 ZILIKUWA NA NAMBA AINA MOJA AMBAYO NI AK S802330 NA NOTI 57 ZILIZOSALIA NAZO ZOTE ZILIKUWA NA NAMBA AINA MOJA AMBAYO NI AK S802338.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA HUYO PAMOJA NA KIASI HICHO CHA FEDHA KUMEKUJA MARA BAADA YA JESHI HILO KUPATA TAARIFA TOKA KWA WANANCHI WEMA AMBAO WALINASA UWEPO WA NOTI HIZO BANDIA NA HATIMAYE TAARIFA KUZIFIKISHA KATIKA JESHI HILO LA POLISI, NALO BILA AJIZI LIKAFANYA KAZI YAKE.

MTUHUMIWA ANASHIKILIWA NA JESHI HILO NA ANATEGEMEA KUFIKISHWA MBELE YA MAHAKAMA.

SIJAELEWA......."

KAKA NDO IMETOKA HIVYO-O! FULL TANK VUUUMmm! STREET.

....MARA TENA KISIKI HIKI CHA MTI KIKAZUNGUSHIWA UZIO, NAONA SASA KINAFUNGULI KIMTINDO INGAWA SIYO RASMI..... SUBIRI TUONE.

HII TOBOA TOBOA KILA NINAYE MWULIZA, ANAJIBU 'SIJUI'.

KWANINI KUNA TOFAUTI KATI YA MA-FIRST LADY WETU NA MA-FIRST LADY WA MBELE?

WOULD ANY FIRST LADY HAVE CHANCED IT?
THAT'S NFL COMMISSIONER...,ROGER GOODELL AND FORMER NFL COACH OF THE YEAR, TONY DUNGY IN THE BACKGROUND.

RUKA RUKA RUKA......

MCHEZO WA UKWELI....

HATUA NYINGINE KATIKA MCHEZO....

FIRST LADY ANAONEKANA SAAAAAAFI, AKILI IKIWA IMEFUNGUKA, AKIWA TAYARI SI KWA MCHEZO TU! HATA KWA MAJUKUMU YA KITAIFA....

HATA MWILI HAUONGOPI, MAMA ANACHEZA KAMA MCHEZA WA UKWELI....

JUMPS ZA KUFA MTU....

SKWATI ZA NGUVU AKA KICHURACHURA....

KIMBIA ILE KINOMA-NOMA....

MWISHO WA MCHEZO JASHO JINGI, SUMU TUPA KULE.....

NA SASA NI KWA MA-FIRST LADY WETU.....ZZzzzzzzzzzz!!!
SOUTH AFRICAN 1st/2nd/3rd LADIES WAKIUCHAPA USINGIZI KWENYE MOJA YA SEMINA MUHIMU NCHINI HUMO.

COME TO THINK OF IT, HOW WILL IDA AND LUCY FARE IN THE GYM ANYWAY!?


THANX KWA MDAU
SAID KASSIM SAID
TPRI ARUSHA.

Wednesday, November 17, 2010

NI NANI MWANASOKA BORA WA BBC 2010?

JEH! NANI KATI YA HAWA:-ASAMOAH GYAN, ANDRE AYEW, SAMWEL ETO'O, YAYA TOURE AU DIDIER DROGBA?

Una nafasi ya kuamua bingwa atakuwa nani, kati ya sasa hadi tarehe 10 mwezi Disemba, na mshindi atatangazwa wiki moja baada ya hapo, Ijumaa ya tarehe 17 mwezi Desemba, katika matangazo ya moja kwa moja ya michezo kwa lugha ya Kiingereza, Fast Track, saa 1600 GMT.

Hili ni tuzo la pekee linalosifika na ambalo hutoa nafasi kwa wewe kama shabiki kuamua mshindi. Mshindi wa mwaka jana alikuwa ni mshambulizi wa Chelsea, Didier Drogba, na ambaye pia huichezea timu ya taifa ya Ivory Coast.

Unaweza kushiriki kwa kupiga kura kupitia mtandao, au kwa kuandika ujumbe wa SMC.
Shughuli ya upigaji kura itaanza saa 1700 GMT, Jumatatu, tarehe 17 Novemba, na itafungwa saa 1700 GMT, Ijumaa, tarehe 10 Desemba 2010.

Kura za mtandao na zile za ujumbe wa SMS zitachanganywa na kuhesabiwa pamoja, na matokeo ya mshindi yatapatikana katika tovuti ya 'BBC African Fooballer of the Year', ambao pia ina masharti mbalimbali na vikwazo vyote vya kushiriki katika upigaji kura.


ZAIDI JINSI YA KUSHIRIKI SIKILIZA BBC SWAHILI.

EID MUBARAK.


NI MUDA MUAFAKA KATIKA MWAKA KUJUMUIKA PAMOJA KULA CHAKULA NA WATU WOTE WA JAMII INAYOTUZUNGUKA. NAAM! NDANI YA SIKUKUU HII IMEHALALISHWA KUCHINJA, HIVYO KWA WALE WENYE UWEZO INSHAHLAH NI VYEMA KUSHIRIKI KUTIMIZA IBADA.
GLOGU YAKO ILIYOMSTARI WA MBELE KTK JUKUMU LA KUANGUSHA NEWS' (g sengo)INAPENDA KUTOA SALAMU ZA SIKUKUU YA EID KWA WAISLAM WOTE AMBAO WANAUNGANA NA WAISLAM KOTE DUNIANI KUADHIMISHA IBADA YA SIKUKUU YA EID-UL-ADHA.

ASSALAMU ALAIKUM WA RAHMATULLAHI WA BARAKATUH !! SHEREHEKEA VYEMA EID-UL-ADHA.

Tuesday, November 16, 2010

BREAKING NEWS! RAIS KIKWETE AMTEUA PINDA KUWA WAZIRI MKUU. BUNGE LAMPA ASILIMIA 84.5

MH. PINDA KWELI UNATOSHA NA UNAENEA KUIMILIKI NAFASI HII.

HATIMAYE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEMTEUA MH. MIZENGO PINDA MBUNGE WA JIMBO LA KATAVI, KUWA WAZIRI MKUU KWA AWAMU NYINGINE. SPIKA MPYA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. NDANI YA UKUMBI WA BUNGE MH. ANNA MAKINDA ALIFUNGUA BAHASHA NA KUISOMA BARUA TOKA KWA MH. RAIS IKIMTAJA PINDA KUWA NDIYE.

KUPITIA KURA ZA PAPO KWA HAPO TAYARI WABUNGE WAMEMTHIBITISHA WAZIRI MKUU HUYO AMBAPO MWANASHERIA MKUU MH. FREDERICK WEREMA AMESOMA MATOKEO YA KURA KAMA IFUATAVYO:- KURA ZILIZOPIGWA 328, ZILIZOHARIBIKA 2 SAWA NA ASILIMIA 0.6 KURA ZA HAPANA 49 SAWA NA ASILIMIA 14.9, KURA ZA NDIYO NI 277 SAWA NA ASILIMIA 84.5.

WAZIRI MKUU ANATARAJIWA KUAPISHWA KESHO IKULU NDOGO YA CHAMWINO, IKIWA NI HATUA YA KWANZA KABLA YA KUTANGAZWA KWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI. HATUA HII INAKAMILIKA BAADA YA RAIS KUKAA NA KUSHAURIANA NA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU.
BARAZA HILO JIPYA LINATARAJIWA KUTANGAZWA IJUMAA.......


Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiteta na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na aliyekuwa Mbunge wa Karatu kabla ya uchaguzi (oct 2010), Dr. Wilbroad Slaa kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma, Aprili 13, 2010. Bunge lilihamia katika ukumbi huo baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya wa Bunge kupata hitilafu.

MCHUJO WA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010 NI JUMAMOSI HII SAA SITA MCHANA

Mchujo wa kuwatafuta wanamitindo wenye sifa za kitofauti yaan i" Giaffe unique model " utafanyika jumamosi hii ya tarehe 20 mwezi wa kumi na moja katika hoteli yenye hadhi ya nyota nne Giraffe ocean view hotel katika ukumbi wa jet 1.

Akiongea na blog zote maarufu nchini Tanzania mratibu wa shindano hilo bwana Magese Methuselah Magese amesema kuwa shindano hilo ni la kizalendo lenye nia mahususi ya kukuza tasnia ya mitindo na wanamitindo wachanga nchini Tanzania kwa kuleta umoja,mafanikio na kuhimiza mapinduzi ili tasnia hii iwe ajira kamili kwa wanamitindo wa hapa nchini kinyume na ilivyo sasa.

Ameongeza kuwa ikiwa vyombo vya habari vitaunga mkono mapinduzi haya kwa kutangaza kwa wingi habari za mitindo, wamamitindo na wabunifu wa ndani, itageuza mtazamo wa watanzania wengi kuondokana na utamaduni wa kuvaa nguo kutoka nje ya nchi pekee badala yake wapende kuvaa nguo zilizobuniwa na wabunifu wa Tanzania.

" Hii itachangia wabunifu kuwa na kipato kikubwa na maonyesho ya mavazi yatakuwa mengi ambapo wanamitindo watafaidika kwa kulipwa kwa kiwango chajuu, aidha vyombo vya habari vikitangaza sana tasnia hii jamii itapenda zaidi hata makampuni mengi yatajitokeza kuwekeza na kujitangaza kwa kudhamini shughuli za mitindo nchini Tanzania kitu ambacho kitaongeza pato la taifa na kpato cha mtu mmojammoja.

Wito umetolewa kwa wasichana wote wenye sifa na vigezo vya kushiriki shindano hilo lenye hadhi ya kitaifa kujitokeza kwaajili ya mchujo tarehe 20 novemba saa sita mchana katika hoteli hiyo iliyopo maeneo ya africana mbezi beach ambapo majaji watakuwa Steven Kanumba, Miriam Gerald, Ali Remtulah, Vitoria Martin na Asia Idarous, watakao shiriki kuchagua wasichana kumi bora wataoingia moja kwa moja katika shindano hilo.

Monday, November 15, 2010

TP MAZEMBE KLABU BINGWA BARANI AFRIKA.

TP MAZEMBE KUTOKA CONGO NDIYO MABINGWA WA LIGI YA MABINGWA BARANI AFRIKA KWAMARA YA 4. HII NI BAADA YA KUSABABISHA SARE YA BAO 1 NA KLABU YA TUNISIA, ESPERANCE KATIKA MCHUANO WA DURU YA PILI YA FAINALI KUFUATIA USHINDI WA MAGOLI 5-0 MCHUANO WA KWANZA MJINI LUBUMBASHI.

MASHABIKI WA TUNISIA WAKIFANYA VURUGU.

KABLA-YA MCHUANO HUO KUANZA POLISI WALIFANYA KAZI YA ZIADA KUZUIA GHASIA ZILIZOANZISHWA MA MASHABIKI WA ESPERANCE WALIORUSHA CHUPA ZA MAJI UWANJANI WAKATI MAZEMBE IKIINGIA. EXP ILIHITAJI MIUJIZA KUSHINDA ZAIDI YA GOLI 5.
MAZEMBE INAJISHINDIA ZAWADI YA DOLLAR MILIONI 1.5 PAMOJA NA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA LA VILABU NCHINI ABU DHABI MWEZI UJAO IKIFUNGUA DIMBA NA KLABU BINGWA YA MEXICO, PACHUCA.

MAMBO YA WIKIENDI' UKISIKIA PAAAH! UJUE ....

INGAWA WALIBAMIZA VICHWA KWENYE KIOO CHA MBELE, WAKIWA NZWII' HUKU WAKIWA WAMELOA CHUZI LA MAPANKI' JAMAA WALIOKUWEMO HUMU NDANI WALITOKA WAKIANGUA VICHEKO NA KUTOKOMEA PASIKO JULIKANA. AJALI HII ILITOKEA JUMAPILI SAA MOJA NA.. ASUBUHI.

INAVYOSEMEKANA WALIKUWA WAMETOKA KULA RAHA TOKA MOJA YA KUMBI MAARUFU KIRUMBA JIJINI MWANZA, KATIKA KUOVATEKI KUSHOTO WAKALIVAMIA ROLI LA KUBEBA MABAKI YA SAMAKI LILILOKUWA LIMEPAKI ENEO LA NERA, LIKISUBIRI PAKUCHE LIPATE KUFANYIWA MATENGENEZO.

ROLI HILI LIKIWA LIMETIMIZA MASHARTI YOTE KAMA KUWEKA ALAMA ZA TAHADHARI, LILIGONGWA KWA NYUMA BILA KUUMIA HUKU LIKIINYEA TAX ILIYOLIGONGA MABAKI YA SAMAKI YENYE HARUFU KALI.

MABAKI YA SAMAKI MARA BAADA YA KUONDOLEWA MINOFU (MAPANKI) YANAYOPELEKWA ENEO MAALUM KUKAUSHWA KUFANYWA CHAKULA KWA KUKU, HARUFU YAKE SI MCHEZO.