ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 11, 2010

MISS TANZANIA ATAKAYE WAKILISHA KTK MISS WORD KUPATIKANA USIKU WA LEO. STAR TV KUONYESHA TUKIO ZIMA LIVE.


NI USIKU WA LEO MABINTI 31 KUKUTANISHWA KATIKA KILELE CHA KUMTAFUTA VODACOM MISS TANZANIA 2010. YUKO WAPI KATI YA HAWA PICHANI?

* Date of the event – September 11, 2010
* Venue of the event – Mlimani city Conference Hall, DSM
* Time of the event – From 7pm sharp onwards
* Tickets selling points – Vodashop Ohio street, Miss Tanzania offices at Mkwepu street, Steers at City Centre, Best Bite Namanga, Rose Garden Bar Mikocheni, Photo Points at Benjamin Mkapa Building City Centre and Mayfair Plaza Mikocheni,
* List of entertainment – Wahu from Kenya, AY, THT group (Barbana, Linah & Mataruma), The Tanzanite band, Chege and Temba.

MAREKANI KUADHIMISHA MASHAMBULIZI YA SEPTEMBER 11.

Sherehe zitafanyika leo nchini Marekani kuadhimisha mashambulizi ya Septemba kumi na moja miaka tisa iliyopita, ambapo watu karibu elfu tatu waliuwawa.

Maadhimisho ya mwaka huu yamegubikwa na utata unaondelea juu ya mipango ya kujenga kituo ca kiislam karibu na viwanja vya mashambulizi hayo mjini New York, na tishio, ambalo sasa limesitishwa, la kasisi wa kanisa moja ndogo katika jimbo la Florida kutaka kuchoma moto nakala za kitabu cha Koran.

Mwandishi wa BBC mjini New York amesema maadhimisho ambayo kwa kawaida hufanyika kwa huzuni mwaka huu yanaelekea kuwa yenye utata mkubwa, pamoja na maandamano ya kuunga mkono na yenye kupinga ujenzi wa kituo cha kiislam yatakayoanza punde baada ya maadhimisho kumalizika.
Rais Obama ametoa wito kwa Wamarekani kudumisha heshima kwa imani za kidini za watu wengine, wakati mataifa ya Kiislam yakionyesha upinzani mkali juu ya tishio la kanisa dogo la Kimarekani kutaka kuchoma moto kitabu cha Koran.

Bw Obama alisema kuchoma maandishi ya kidini ni kinyume na maadili mema ambayo ndiyo msingi wa Marekani.

Kasisi anayetaka kutekeleza kitendo hicho, Terry Jones, amesema amesitisha mpango wake wa kuchoma Koran wakati wa maadhimisho ya mashambulizi ya Septemba kumi na moja , lakini anataka kukutana na Imam anayesimamia mpango wa kutaka kujenga kituo cha kiislam karibu na eneo la jengo lililoangushwa katika mashambulizi hayo la World Trade centre mjini New York.

Friday, September 10, 2010

NI KIWEWE IKIWA KASISI MMOJA ATACHOMA QURAN.

Kasisi wa Kimarekani ambaye amezua lalama kali duniani kufuatia mpango wake wakuchoma Koran tukufu hapo Kesho Septemba 11 amesema mpango wake utategemea kutekelezwa kwa masharti anayotaka yafanywe.

Saa chache zilizopita, Mchungaji Terry Jones alitangaza kufutilia mbali mpango wake wa kuchoma moto nakala za Koran tukufu

Hii ilikuwa baada ya kudai kwamba alikuwa amefikia makubaliano na viongozi wa kiislamu.Alidai walikubaliana kubadili sehemu ya kujenga kituo cha kiislamu, mjini New York, ili naye mchungaji huyo afutilie mbali uamuzi wake wa kuchoma moto nakala za kitabu cha Koran.
Jones aliandamana na Imam wa eneo lake akitoa tangazo hilo.


"Raia wa Marekani hawataki msikiti pale na bila shaka waislamu hawataki sisi tuchome Koran. Imam amekubali kuhamisha mpango wa kujenga kituo cha utamaduni cha kiislamu, katika eneo ambako mashambulio yalifanyika"Alisema Jones.

Hata hivyo si wazi kama makubaliano yamefikiwa. Msemaji wa kundi linalohusika na ujenzi wa kituo hicho amesema kuwa hakuna mpango wowote wa kuhamisha kituo hicho na msikiti.

Bw Jones anadai kuwa viongozi hao wa kiislamu walimhadaa.

Huenda kile mchungaji Jones anachosema ni makubaliano, ni mazungumzo tu kwamba yeye na Imam wa New York, Faizal Rauf, ambaye ndiye msimamizi wa mradi huo watakutana jumamosi kujadili, hali ambayo bado ni ya utata kuhusu ujenzi wa kituo hicho.

Awali, katika mohojiano na kituo cha televisheni cha ABC, rais Obama alitaja mpango wa mchungaji huyo kama mchezo wa kuigiza.

"Kama anasikiliza natumaini anaelewa kwamba kile anachopendekeza kukifanya, ni kinyuma kabisa na maadili yetu kama wamarekani. Kwamba nchi hii ilijengwa kwa misingi ya uhuru wa kuabudu na kuvumiliana kwa dini. "alionya Obama.

Kitendo cha mchungaji huyo kutaka kuchoma moto kitabu cha Koran kimeshutumiwa vikali kote duniani.


KWA HISANI YA BBC SWAHILI.

FBME BANK LTD KANDA YA ZIWA WATOA SWADAKA KWA YATIMA MWANZA

Wafanyakazi wa bank ya FBME kanda ya ziwa wakiwa pamoja na uongozi wa kituo cha kulea watoto cha Islamic Yatima Foundation kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Baadhi ya Swadaka zikikabidhiwa kwa watoto yatima wa kituo cha Ilemel na Joseph Gwalugano na Maulid Tarimo.

Wakiongozwa na meneja wa tawi la Mwanza Bw. Joseph Gwalugano, walikabidhi swadaka yao kwa uongozi wa kituo hicho. Kutoka kulia ni Peter Nkenguye, Rehema Mbalike, Allawi Mdee (Afisa Maendeleo ya Biashara wa tawi) Mkuu wa shule ya msingi, na Joseph Gwalugano (meneja wa tawi ).

Afisa Maendeleo ya Biashara wa tawi hilo akimkabidhi mtoto Osama swadaka ikiwa ni zawadi yakuwa kati ya washindi wa kuhifadhi Quran tukufu kanda ya ziwa.

Annah Lupemba, mmoja wa maafisa wa tawi hilo akikabidhi swadaka kwa watoto hao wa Islamic Yatima Foundation

Wafanyakazi hao wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhi swadaka zao kwa watoto yatima wa Ilemela – Mwanza.

TUSHEREHEKEE IDDI KWA AMANI, UPENDO NA FURAHA, HUKU TUKIPEANA ZAWADI.

'RAFIKI TUPEANE MKONO WA IDDI'
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKISALIMIANA NA BAADHI YA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU MUDA MFUPI BAADA YA KUMALIZIKA KWA SWALLA YA IDDI ILIYOSWALIWA KATIKA MSIKITI MKUU WA RIYADHI MJINI TANGA KITAIFA LEO ASUBUHI.

MDAU UMEIONA OFA HII KABAMBE KUTOKA VODACOM?

IKIWA LEO NI SIKUKUU YA EID EL FITRI, SOKO LA MWALONI ASUBUHI YA LEO LIMEKUWA KIMYA TOFAUTI NA ILIVYOZOELEKA, NAJUA WAJUA.

BARABARA ZOTE JIJINI MWANZA ASUBUHI YA LEO NIMEZISHUHUDIA NI NJIA MOJA TU KWENDA KUHUDHURIA SALA YA EID. KILA LA KHERI KWA NDUGU ZANGU WAUNGWANA.

Thursday, September 9, 2010

MRADI WA CHAMPION WATETA NA WADAU JIJINI MWANZA MENGI YAIBULIWA, WADAU WAJIFUNZA.

ULE MRADI UNAUNAOLENGA KUHAMASISHA MJADALA WA KITAIFA KUHUSU MAJUKUMU YA WANAUME NA KUONGEZA USAWA WA KIJINSIA HIVYO KUPUNGUZA HATARI YA WANAUME, WANAWAKE NA WATOTO KUPATA VVU\ UKIMWI NA KUPUNGUZA MATOKEO YA ATHARI ZINGINE MBAYA ZA AFYA YA UZAZI, MRADI HUO LEO UMETINGA JIJINI MWANZA KUZUNGUMZA ANA KWA ANA NA WADAU WA HABARI.

KAMPENI YA MAWASILIANO BAINA YA WAPENZI IMEANZISHWA BAADA YA TAFITI KUFANYWA NA KUONYESHA KUWA KUNA TATIZO LA MAWASILIANO BAINA YA WATU WALIOPO KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI KAMA NDOA TATIZO LINALOPELEKEA KUTORIDHIKA HIVYO KUWA NA MAHUSIANO NA WAPENZI WENGI CHANZO CHA MAAMBUKIZI YA VVU.

KWA NINI INAFIKIA WAKATI UNAJUTA KUZALIWA MWANAMKE?
MAJIBU YA WENGI:
-pingamizi ya haki hata kama ni juu ya suala dogo lenye maamuzi juu ya mwili wako.
-kutokuwa na maamuzi katika familia pindi nitakapoolewa.
-nabeba mimba nailea, mtoto anazaliwa, nasimamia malezi mpaka anakuwa mwisho wa siku nikiachana na mwanaume 'mtoto mali ya mwanaume'


MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA BEATRICE NAYE ALIREJEA NYUMBANI MWANZA KUUNGANA KUHAMASISHA JUU YA MPANGO MZIMA WA KUVUNJA UKIMYA.

MAMBO MENGI YALIIBULIWA KATIKA MDAHALO HUO, HITIMISHO LIKAWA:
-mawasiliano ni muhimu katika kudumisha upendo na furaha ktk mahusiano.
-mawasiliano mazuri hujenga ushirikiano ktk familia.
-mawasiliano mazuri ni yale yenye uwazi kuthaminiana na kusikilizana.


UNGEJIBUJE KWA SWALI HILI: JE UNAJUTA KUZALIWA MWANAUME?

MR MATAGIRI TOKA MPANGO WA KULINDA ZIWA VICTORIA AMECHANGIA KUWA MILA NA DESTURI NA KUOGOPA KUONEKANA KAMA SIYO MWANAUME NI MOJA YA VIKWAZO KATIKA MAWASILIANO.

PICHA YA PAMOJA WADAU WA CHAMPION MWANZA WALIO FANIKISHA ZIARA HIYO.

Wednesday, September 8, 2010

Mamia ya wafungwa wametoroka jela NIGERIA.

Mamia ya wafungwa wametoroka jela moja iliyo eneo la kati la Nigeria baada ya genge lenye silaha kuvamia gereza.

Wakuu wa Nigeria wanadai kuwa kundi lenye msimamo mkali wa Kiislamu, Boko Haram ndilo lililohusika na shambulio hilo.

Imethibitishwa kuwa watu wanne waliuawa na wengine sita kujeruhiwa.

Polisi sasa wanasaka baina ya watu mia saba na mia nane katika Jimbo la Bauchi.

Wahalifu hao wenye silaha walivamia jela na kuingia kila chumba wakiwaachilia huru wafungwa kabla ya kulichoma moto jengo zima la gereza.

Wakuu hao wanasema taarifa za kijasusi zinaonyesha kuwa kundi la Boko Haram lenye msimamo mkali unaopinga elimu ya magharibi na sayansi ndilo lililohusika.

Takriban wafuasi 100 wa kundi hilo walikuwa ndani ya jela hiyo wakisubiri hukumu kutokana na ghasia za mwaka jana dhidi ya polisi na serikali ya Nigeria.

Wakati huo zaidi ya watu 800 waliuawa na kiongozi wa kundi hilo Mohammed Yousef akauawa kwa risasi baada ya kuizingira nyumba yake.

Lakini katika siku za hivi karibuni kundi hilo limejigamba kuwa na kiongozi mpya na kwamba lina mipango ya kujiimarisha kwa silaha.

Kuna khofu kwamba kundi hilo linatumia mbinu mpya na ujanja na huenda limehusika katika 'mawaji baridi' ambamo maofisa kadhaa wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha wakitoroka kwa kutumia kasi ya pikipiki.


KWA HISANI YA BBC SWAHILI.

MMMH!

KINOTISI KWA WAZEE WA MIZINGA.

MWANVULI WA NINI? MTAJI WANGU WENYEWE KIKINGA MVUA.

UPO HAPO? HII NI BEI YA VYAKULA (MENU) KATIKA KIJIJI CHA NYAMILAMA TARAFA YA MALAMPAKA WILAYANI MASWA MKOANI SHINYANGA, TENA HAPO NDIYO MABADILIKO YA BEI NDO IMEPANDA HIVYOO.

PERFECT KASIGA A.K.A P.DIDDY AFARIKI GHAFLA

HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE NA ZA KUTHIBITIKA KABISA, ZINARIPORI KWAMBA MKURUGENZI MSAIDIZI WA BENDI YA MUZIKI WA DANSI YA DIAMOND MUSICA, PERFECT KAGISA 'P. DIDDY' (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA.

P. DIDDY AMBAYE ALIKUWA NI MCHUMBA WA MTANGAZAJI MAARUFU WA TBC1,MAIMATHA JESSE AMEPATWA NA MAUTI HAYO LEO HII WAKATIKA AKIWA KATIKA MATEMBEZI YAKE YA KILA SIKU BAADA YA KUANGUKA GHAFLA KATIKA BARABARA YA LUMUMBA, MNAZI MMOJA, JIJINI DAR ES SALAAM

MWILI WA MAREHEMU UMEPELEKWA KATIKA HOSPITAL YA TAIFA YA MUHIMBILI KWA UCHUNGUZI ZAIDI.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN


KWA HISANI YA MICHUZI JR.

Tuesday, September 7, 2010

'STONE CLUB' SWAG ON SIKUU YA EID EL FITRI.

BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU NA WATU KUPATWA NA GONJWA JIPYA UBUNA (UPUNGUFU WA BURUDANI NAFSINI), ILE CLUB YAKO IMERUDI TENA NA SAFARI HII NI ZAIDI.

FUNDI AKINAKSHI SEHEMU ZA KUTA NDANI YA UKUMBI WA STONE CLUB ROCK CITY AMBAPO UFUNGUZI RASMI KUFANYIKA EID MOSI, DJ MWALIKWA DJ PQ KULIGENGESHA.

MBALI NA KUWA NA MWONEKANO WA UTOFAUTI NA ULE ULIOZOEA, STONE CLUB KWA SASA ITAKUWA NA SOUND YA UKWELI, LIGHTS ZIMEFUNGWA MPYA, ZILE ZA ZAMANI TUPA KULEE, DANCE FLOW TAMU, KAUNTA KONA ZOTE TANO, SMOKING CHAMBER, WASH ROOM ZA KISASA, AIR CONDITION NA.....

NIMEVAMIA TU! KAZI IKIKAMILIKA UTAUFAIDI MWONEKANO.

MISHEMISHE KAMANGA FERRY

SAFARI NYINGI ZA MV VICTORIA TOKA BUKOBA HADI MWANZA MBALI YA KUTUMIKA KAMA USAFIRI WA WATU NA MIZIGO KWA KIASI KIKUBWA USAFIRI HUO UMEKUWA UKITUMIKA KUSAFIRISHA MAZAO YA BIASHARA.

HIVYO KULIFANYA ENEO LA KAMANGA FERRY KUWA BIZE KWA BIASHARA HUSUSANI SIKU ZA SAFARI ZA MELI.

WENYEJI WA MKOA WA KAGERA KULA UGALI AU WALI MFULULIZO KWAO NI UMASKINI, NDIZI (MATOKE) NDIYO CHAKULA CHAO KIKUU NA MAPISHI YAKE EH BANA DAAH! LAZIMA UJIRAMBE, HUMO NDANI MCHANGANYIKO WA MAHARAGE, NYAMA NA MBOGA MBOGA. PICHANI NDIZI MBIVU.

KAMA NI MZIGO MKUBWA WA NDIZI (SHEHENA)KWAAJILI YA BIASHARA MIKOA MINGINE TANZANIA NA NCHI JIRANI, NDIZI HIZO HUSAFIRISHWA KWA MITUMBWI NA MAROLI HIVYO MZIGO UNAO SAFIRISHWA NA MELI YA MV VICTORIA MARA NYINGI HUWA MAHSUSI KWA BIASHARA YA NDANI MKOA WA MWANZA NA WILAYA ZAKE. PICHANI HII NI SEHEMU MAHUSUSI KWA WAFANYABIASHARA WA NDIZI REJEREJA.

SI NDIZI PEKEE BALI KUNA MAHARAGE, KAHAWA NI BAADHI YA MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA AMBAYO HUTOKA MKOA WA KAGERA NA KUPITA HAPA.

Monday, September 6, 2010

MWANZA BY NIGHT.

AL MASJID.

KEEP LEFT AT CITY CENTRE.

MWANZA PORT.

MAKONGORO ROAD.