ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 14, 2010

MWANZA YAONDOKEWA NA MSANII: NI HAMAD SALEHE WA BWV.

MAREHEMU HAMAD SALEHE KATIKA FIESTA 2004 CCM KIRUMBA MWANZA.
Kama waijua vyema historia ya muziki wa Bongo Fleva kwa mkoa wa Mwanza hakika utakuwa unawafahamu wasaii kama Jontwa Jokeli, Jose Kashushura, Phantom Lanks, Shija Rweymamu, jingo Man, Jet Man, Jitah Man, Kid Bway na wengine wengi waliokuwa wakitikisa katika muziki huo wa kizazi kipya miaka ya tisini na mwanzoni mwa millennium mpya katika kona ya muziki wa Ragga. Na katika hip hop kuna wengi Fid Q ‘Ngosha the Don’ anayetamba hadi sasa, Dr KB na bila kusahau kundi la BWV ambapo humo nina tuama nikiwa na Inshu ya kuzungumzia.
WAKIWA CITY CABANA MWANZA KUTOKA KUSHOTO WALIO CHINI NI BAVON, AMBWENE YESAYA 'AY' NA PHILBERT KABAGO NA WALIOSIMAMA KUTOKA SHOTO NI MAREHEMU HAMAD SALEHE, DR LIFE NA HAYATI COMPLEX.
BWV au BOYS WITH VOICES ni kundi lililoundwa na vijana wawili Filbert Kabago na Hamad Salehe waliochangia harakati za Maendeleo ya jiji la Mwanza pale walipopakuwa singo iitwayo ‘barabara’ ikichambua uhalali wa Mwanza kuitwa jiji ile hali Barabara zikiwa tope na mahandaki kibao, changamoto hiyo iliigusa serikali hata ikafanya mambo hatimaye miaka ya sasa twaziona barabara za jiji la mwanza zikiwa full mikeka.
MWENYE KIPAZA MBELE NI MAREHEMU HAMAD SALEHE KWENYE UZINDUZI WA ALBUM YAO BWV CCM KIRUMBA SEPTEMBER 14/2003 ULIOANDALIWA NA ZIZOU FASHION (TIPPO) ENZI HIZO H.BABA AKIWA DENSA.
BWVWalijali pia maslahi ya wafanyakazi pale walipoiweka hewani singo ‘Bosi nipe mshahara wangu’ track iliyo bamba na kushika wengi, kwa wafanyakazi wakiitumia kama mkombozi wa haki zao huku waajiri wasio zingatia majukumu yao wakizima radio kutokana na madongo yaliyokuwa yakielekezwa kwao.
Nazungumza YOTE haya kukupa TU! historia ujue japo kwa muhtasari muziki wa kizazi kipya mkoa wa Mwanza ambao ni moja kati ya mikoa iliyotia changamoto kwa muziki Bongo fleva kukuwa nchini Tanzania. Nayatanguliza maelezo hayo nikiwa na masikitiko kutangaza kifo cha Hamad Salehe mmoja kati ya vijana waliounda kundi la BWV.

STUDIO ZA MWANZA RECORDS KWA ENRICO FEGWERADO: KUTOKA SHOTO NI SOGGY DOGGY, PHILBERT KABAGO NA HAMAD SALEHE NA SISTER P (PALE KATI).
Baada ya kuugua kwa muda mrefu Hamad Salehe amefariki dunia mwishoni mwa juma siku ya jumapili ya Tarehe 12 dec 2010 saa 8 mchana na kuzikwa jumatatu ya tarehe 13 dec 2010 kabla ya adhuhuri katika makaburi ya kirumba jijini Mwanza. Akizungumzia kuhusu msiba huo msanii mwenzake katika kundi Philbert kabago anayetamba na singo Wivu aliomshirikisha mwanadada Farida anasema kuwa ingawa kwa kipindi kirefu amekuwa akifanya muziki kama solo kutokana na msanii mwenzie kuugua pengo alikuwa analiona lakini kwasababu hakuwa na jinsi ilimbidi kupigana hivyo hivyo. Marehemu Hamad Salehe alizaliwa juni 23 1982 Nyakalilo wilayani Sengerema, akianza muziki mwishoni mwa 1996 akiwa darasa la sita shule ya Victoria Internation. Marehemu ameacha mtoto mmoja wakiume(6).

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. habari ya kusikittisha...poleni familia ya Hamad,swahiba wake P Kabago na wapenzi wa muziki.Hakika bado namkumbuka vema sama homeboy wangu Hamad..Mwenyezi Mungu wa rehema aipumzishe roho yake mahala pema peponi.Amin

    ReplyDelete
  2. Honsetly inasikitisha sana, sikuwahi kutambua kama Hamad alifariki toka mwaka 2010 Desemba, Ni leo napotafuta icha ya JETMAN ambaye naumwa kwa sasa kwa ajili ya kuhamasisha nguvu za Indegeneous kumsaidia mwenzetu ndio nakutana na picha ya Hamad, Mie nilikuwa namtania Bwana Kimuru Mambo kutokana na kushiriki sehemu hiyo katika VIDEO ya Mshahara wakimshirikisha mwanamama Maua, VIDEO mbayo ni moja ya kazi zangu za mwanzo katika game nikiandika script, kuishot na baadaye Editing katika kiwango cha juu sana.

    Pumzika kwa Aman Kimuru Mambo wote safari ni Moja.

    R.I.P

    With Love

    Yahya Mohamed Kimaro

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.