ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 17, 2010

NI NANI MWANASOKA BORA WA BBC 2010?

JEH! NANI KATI YA HAWA:-ASAMOAH GYAN, ANDRE AYEW, SAMWEL ETO'O, YAYA TOURE AU DIDIER DROGBA?

Una nafasi ya kuamua bingwa atakuwa nani, kati ya sasa hadi tarehe 10 mwezi Disemba, na mshindi atatangazwa wiki moja baada ya hapo, Ijumaa ya tarehe 17 mwezi Desemba, katika matangazo ya moja kwa moja ya michezo kwa lugha ya Kiingereza, Fast Track, saa 1600 GMT.

Hili ni tuzo la pekee linalosifika na ambalo hutoa nafasi kwa wewe kama shabiki kuamua mshindi. Mshindi wa mwaka jana alikuwa ni mshambulizi wa Chelsea, Didier Drogba, na ambaye pia huichezea timu ya taifa ya Ivory Coast.

Unaweza kushiriki kwa kupiga kura kupitia mtandao, au kwa kuandika ujumbe wa SMC.
Shughuli ya upigaji kura itaanza saa 1700 GMT, Jumatatu, tarehe 17 Novemba, na itafungwa saa 1700 GMT, Ijumaa, tarehe 10 Desemba 2010.

Kura za mtandao na zile za ujumbe wa SMS zitachanganywa na kuhesabiwa pamoja, na matokeo ya mshindi yatapatikana katika tovuti ya 'BBC African Fooballer of the Year', ambao pia ina masharti mbalimbali na vikwazo vyote vya kushiriki katika upigaji kura.


ZAIDI JINSI YA KUSHIRIKI SIKILIZA BBC SWAHILI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.