ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 19, 2010

MAADHIMISHO YA SIKU YA CHOO DUNIANI MKOANI MWANZA.

Mila potofu zimetajwa kuchangia kwa asilimia kubwa maambukizi ya maradhi yatokanayo na kukiuka kanuni za afya na usafi, likibainika katika utafiti uliofanywa kwa wakazi wa vijiji vya wilaya ya Magu, ambapo familia moja yenye zaidi ya watu kabla ya kula, hunawa maji kwenye bakuli moja kasha mara baada ya hapo mzee wa familia huyanywa maji hayo kama tiba ya kutanua kifua au humnywesha motto mchanga kwa makusudi hayo ya kumpanua kifua.

Takwimu za vyoo katika jiji la mwanza zinaonyesha kuwa vyoo bora ni asilimia 64%, vyoo duni ni asilimia 33% na nyumba ambazo hazina vyoo kabisa ni asilimia 3%, changamoto ya tatizo hilo ikitajwa kuwa ni pamoja na gharama kubwa ya vifaa vya ujenzi, umasikini na ufukara wa wananchi kutokana na kipato duni na kiwango cha uelewa,na hali ya miamba na baadhi ya maeneo kuwa na chemichemi nyingi hasa mabondeni.

Kwa upande wa matumizi ya vyoo kulingana na hali ya kijiografia na jinsi ujenzi holela milimani ulivyo, imegundulika kuwa siyo kwamba nyumba zote zilizoko sehemu za milima hazina vyoo bali taarifa sahihi ni kwamba vyoo vilivyopo maeneo hayo siyo bora na si vya kudumu.

Sambamba na maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa kila halmashauri nchini huku mkoa wa Tanga yakifanyika kitaifa , halmashauri ya jiji la Mwanza kwa kushirikiana na PLAN INTERNATIONAL imefanya maonesho katika viwanja vya furahisha ya choo rahisi bora na cha kisasa kama darasa kwa wananchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.