ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 14, 2010

TUMUENZI BABA WA TAIFA KWA VITENDO.


TAIFA LA TANZANIA LEO LINATIMIZA MIAKA 11 TOKA KIFO CHA MUASISI WAKE BABA WA TAIFA HAYATI JULIUS KAMBARAGE NYERERE KILICHOTOKEA KATIKA HOSPITALI YA MT THOMAS LONDON, UINGEREZA AMBAPO WATANZANIA WANAADHIMISHA SIKU HII IKIWA BADO SIKU KUMI NA SABA KUFIKIA UCHAGUZI MKUU OCT 31/2010.

VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI VIMEENDELEA KUKUMBUSHA HOTUBA ZA MWALIMU, MOJA KATI YA HOTUBA HIZO NI ILE INAYO TUASA JUU YA KIONGOZI GANI BORA KUMCHAGUA SIKU YA KUPIGA KURA. KARIBU MANENO MENGI KWENYE HOTUBA ZINAZORUSHWA HEWANI NA VYOMBO VYA HABARI VYA KIELEKTRONIKI YAMETENDEKA NA NDIYO MAMBO YANAYOZUA GUMZO KTK JAMII YA WATANZANIA KWA SASA.TUKIO LA LEO LINAKWENDA SAMBAMBA NA HITIMISHO LA MBIO ZA MWENGE WA UHURU.
JUHUDI ZA MAENDELEO ZINAANZIA PALE ULIPO NA KWA KILE KIDOGO ULICHONACHO.“Tanzania inatakiwa kufahamu kuwa misingi sahihi ya nchi yetu imejengwa kwa nguvu kubwa na waasisi wa taifa letu hivyo wale wote wanaotaka kuibomoa wanakosea na wanafanya dhambi kubwa na ipo siku watahukumiwa kwa kuwa hakuna anayependa kuona nchi inagawanywa kwa sababu wachache wanataka kuona wanapata furaha huku wengi wakiumia.”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.