ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 27, 2010

TUKIO LA MAUAJI NA UPORAJI UKEREWE, JAMBAZI MOJA LAKAMATWA.

MNAMO TAREHE 24/10/2010 MAJIRA YA SAA 20:00 HUKO KATIKA KISIWA CHA NANSIO UKEREWE KATIKA ENEO LA KISIMA CHA MAFUTA KINACHOMILIKIWA NA MFANYABIASHARA CHACHA KANENE (43), KUNDI LA WATU WA 5 WAKIWA NA BUNDUKI MOJA AINA YA SMG NA MAPANGA WALIWAVAMIA WALINZI NA WAFANYAKAZI WA KITUO HICHO CHA MAFUTA NA KUWATEKA KISHA KUMUUA MAREHEMU JITIHADA IBRAHIM MWAIPOPO NA KUMJERUHI KWA KUMPIGA RISASI YA KISIGINO MGUU WA KULIA BW. CLEOPHAS HAMISI AMBAYE NI MTEJA DEREVA WA PIKIPIKI NO T811BGA.

MBINU ILIYOTUMIKA NI KUWATEKA WALINZI NA WAFANYAKAZI WA KITUO HICHO NA KUPORA SH. 1,200,000/= ZIKIWA NI MAUZO YA SIKU KUANZIA SAA 10 JIONI HADI MUDA HUO SAA 2 USIKU.

MARA BAADA YA TUKIO HILO KUFIKA KITUO CHA POLISI UKEREWE, POLISI WALIANZA UFUATILIAJI NA MNAMO TAREHE 25/10/2010 IKIWA NI SIKU YA PILI MARA BAADA YA TUKIO WALIFANIKIWA KUMKAMATA FRANSIS BHOKE AKA MASELO (33) KABILA MKURYA MKAZI WA KIJIJI CHA MAGOLO TARIME MKOANI MARA AKIWA NA BUNDUKI AINA YA SMG YENYE NAMBA 56-390-10-27 IKIWA NA MAGAZINE YENYE RISASI 10 NDANI, MAKASHA MATATU YALIYOTUMIKA, MAPANGA MANNE, MAKOTI MATATU NA KOFIA TATU AINA YA SOX VYOTE HIVI VIKIWA NDANI YA BEGI.

MTUHUMIWA MARA BAADA YA KUKAMATWA NA KUHOJIWA ALIKIRI KUHUSIKA NA TUKIO HILO IKIWA NI PAMOJA NA KUHUSIKA NA MATUKIO YA UJAMBAZI UKEREWE NA MIKOA YA SINGIDA, DODOMA NA ARUSHA.

JESHI LA MKOA WA MWANZA LINATOA PONGEZI KWA WANANCHI WA WILAYA YA UKEREWE KWA USHIRIKIANO WALIOUONYESHA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.