ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 25, 2010

NIMESOMA BANGO PALE ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO' MIE NAUCHAPA USINGIZI SAFARINI!


KATIKA SAFARI YANGU ILIYOANZA YA SAA 12 ASUBUHI HADI SAA 2 USIKU ILITAWALIWA NA USINGIZI HASA NYAKATI ZA MCHANA.

TAMAA YANGU KUBWA ILIKUWA KUPATA PICHA ZA VIJIJI NA MAISHA YA WATANZANIA MKOA KWA MKOA, TATIZO SASA NILIKUWA NASINZIA ILE KINYAMA' NA KILA NIKIZINDUKA BABAKE! NAONA PORI NA MASHAMBA, KWAMBA SEHEMU ZA MIJI TAYARI TUMEZIPITA. 'KUNDA-NDA-NDEKI'

LAKINI NAPATA VITU DIFERENTI' SAFARINI.

MWISHO WA SIKU NIKAWA NAZIJADILI SASA.. PICHA NILIZOPIGA NJIANI NINI KIMESABABISHA KUTOTIMIZA LENGO. jibu likawa: USINGIZI.


KWA KAWAIDA USINGIZI UNACHUKUWA THELUTHI MOJA YA MUDA WA MAISHA YOTE KWA BINADAMU, NA UNAHUSIANA KWA KARIBU NA AFYA YA WATU. USINGIZI BORA NA WAKUTOSHA NI MSINGI MUHIMU WA AFYA. LAKINI WATU WENGI HATUFAHAMU SAYANSI YA USINGIZI KWAMBA BINADAMU ANAHITAJI USINGIZI KWA SAA NGAPI? NI KWA VIPI ANAWEZA KUUBORESHA USINGIZI? INAFAA KULALA MCHANA AU?


JE NI VYEMA KULALA SAFARINI? BILA SHAKA JIBU NI SI VYEMA KWANI VYOMBO VYA USAFIRI VINA TAHADHARI ZAKE, NA NI RAHISI KWA MSAFIRI KUPATA TAARIFA YA TAHADHARI IKIWA ATAKUWA MACHO.

'ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO' HIVYO MSAFIRI NI KAMA MLINZI WA DORIA. KULALA KOSA LA JINAI.

KUHUSU KULALA MCHANA AU ADHUHURI: WATAALAM WANASEMA USILALE KWA MUDA MREFU SANA MAJIRA HAYO, DAKIKA 10 HADI NUSU SAA INATOSHA. KWA SABABU UKILALA KWA MUDA MREFU NA KUINGIA KWENYE USINGIZI MZITO, ITACHUKUWA MUDA KURUDISHA UFAHAMU WA KAWAIDA KUTOKA USINGIZINI KWA KUWA UFAHAMU HUTOWEKA KIKAMILIFU WAKATI WA USINGIZI MZITO.

UMEJIFUNZA JAMBOeeeee!!!!! SEMA NDIYO NDIYO!!

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Uncleeeeeee! Blongu limetulia sana. Big up sana. Tuko pamoja. Usingizi ni dawa muhimu hivyo usilaumu sana. Endelea kuleta vituuzi.

    Magashi S.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.