ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 27, 2010

'WANA HIP HOP' FID Q NA BABA LUKU NDANI! TAREHE 18 SEPT 2010 TUNZA LODGE PATAKUWA HAPATOSHI! BURUDANI NA SANAA KUTAWALA .

ZAIDI ya watoto 50 wanaoishi katika mazingira magumu na wale wanaolelewa katika vituo vya watoto yatima kutoka katika mikoa ya Arusha,Dar es Salaam pamoja na Mwanza wanatarajia kushirika maonyesho ya Earthdance jijini hapa.

BANGO LA KUELEKEZA TUNZA LODGE.

Maonyesho yatafanyika katika nchi 80 maeneo 500 ya nchi hizo ambapo Tanzania itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza katika kufanya maonyesho hayo ambayo huwa yanafanyika kila mwaka Septemba 18.

UFUKWE TULIVU WA TUNZA LODGE.

Mratibu wa maonyesho hayo Ben Mwangi amesema kuwa siku hiyo maalum watu hukusanyika ktk sehemu mbalimbali duniani na kufanya maombi ya amani. Maombi hayo huwa yanaambatana na muziki wa dansi wa asili ambao huwa unalenga kudumisha mila na destuli za makabila husika.

UFUKWE WA ZIWA VICTORIA MAJI BARIDI.

Wasanii wakali wa hip hop kama Fid Q toka TZ na Baba luku toka UGANDA kupamba stage la burudani.Asilimia 50 ya fedha ambazo watazipata katika maonysho hayo kutoka katika kingilio zitaenda kwa watoto yatima wa kituo cha kuleana jijini Mwanza ambapo zitatumika kuwaendeleza katika miradi yao.

TUNZA LODGE KWA NJE.

Wanachi watao udhuria maonyesho hayo watapata fursa ya kuona maonyesho ya mavazi ya kimasai pamoja na kupata fursa ya kupiga picha wakiwa katika mamevaa mavazi hayo ya asili.



NGOMA YA WASUKUMA.

Maonyesho hayo yamedhaminiwa na kampuni ya bia TBL kwa kupitia bia ya Kilimanjaro ambapo zawadi mbalimbali na michezo kuwepo SIKU HIYO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.