ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 7, 2010

MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA AZOMEWA.

PICHANI RAIS JAKAYA KIKWETE AKIPIGA NGOMA ALIPOTEMBELEA ENEO LA MAKUMBUSHO YA KABILA LA WASUKUMA BUJORA NJE KIDOGO YA JIJI LA MWANZA. PEMBENI YAKE MWENYE JOHO NI PADRI SANDU NICASIUS AMBAYE NI KIONGOZI WA MAKUMBUSHO HAYO AKITOA MAELEZO.

HABARI KAMILI:-
ZOMEAZOMEA ya viongozi wa serikali imeendelea kuwakumba viongozi waandamizi, baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, kuzomewa na wananchi mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Kabwe alikumbwa na mkasa huo baada ya Rais kumwita jukwaani na kumtaka atoe maelezo ya kina kuhusu kuwekewa alama za X kwenye baadhi ya nyumba za wananchi wa kata ya Mkolani jijini Mwanza.
Rais Kikwete ambaye yuko ziarani mkoani Mwanza, alitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkolani ambapo pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi huku akiwataka waeleze kero zao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkolani A, Mathias Kihamba, alipewa nafasi na Rais Kikwete kueleza matatizo yanayowakabili ambapo mwenyekiti huo alisema kuwa wanaishi kwa wasiwasi katika nyumba zao kwa kuwa zimewekwa alama ya X pasi sababu za msingi.
Hata hivyo kinyume na matarajio ya wengi mkurugenzi huyo alishindwa kueleza sababu ya kuwekwa alama hizo za X zaidi ya kusema kuwa inawezekana kwa sababu watu wamejenga kiholela au ndani ya hifadhi ya barabara.
Rais Kikwete kusikia zomeazomea ikizidi kushika kasi, aliamua kumuokoa mkurugenzi huyo kwa kumtaka kulifanyia kazi haraka jambo hilo ili kupunguza malamiko ya wananchi.
Rais Kikwete yuko mkoani Mwanza kwa ziara ya siku mbili ambapo alikagua ujenzi wa barabara ya lami ya kutoka Usagara hadi Geita na kusema hakuna barabara itakayosimama kujengwa kwa sababu ya kukosa fedha . Leo Jumapili ametembelea makumbusho ya kabila la wasukuma na baadaye kufungua sherehe za Bulabo.

Tupe maoni yako

3 comments:

  1. jamani lini viongozi wa mwanza watapata elimu?siwezi kusema eti hawana uzoefu wa kazi, sababu kabla ya miaka walipelekwa mahakamani na tajiri aliyevunjiwa kituo cha mafuta na kuamriwa kukilipa. sasa wamewaingilia walala hoi ambao ni chanzo cha fujo zozote zitakazotokea zitawaathiri viongozi hao ambao hawajapata elimu na hawajasoma jiji la mwanza vizuri.

    ReplyDelete
  2. NASIKITIKA NA SINA HURUMA NAYE KUSOMA KUWA MKURUGENZI WA JIJI HAELEWI YANAYOTOKEA KATIKA JIJI NA KUTOELEWA SABABU ZA X KUWEKWA KWENYE NYUMBA HIZO, AU ANAENDESHWA NA WALIO CHINI YAKE. IKIWA HAFAHAMISHWI, INAPASA YEYE KUFUATILIA HIYO NI WAJIBU WA AJIRA YAKE.

    ReplyDelete
  3. mh kazi kweli kweli
    iweje asijue wakati yeye ndie mhusika?

    bm
    uk

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.