ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 19, 2010

VAGI LAZUKA LEO KATI YA MGAMBO WA JIJI NA MACHINGA MWANZA.

<-kioo cha ghorofa ya pili jengo la seif plaza kilichotobolewa na risasi.

LEO MAJIRA YA SAA 5 ASUBUHI IMETOKEA VURUGU BAINA YA MACHINGA NA MGAMBO WA JIJI PAMOJA NA ASKARI POLISI WANAOANDAMANA NA MGAMBO HAO WA JIJI KATIKA ZOEZI LA KAMATAKAMATA.

HALI YA HEWA ILICHAFUKA GHAFLA NA AMANI KUTOWEKA KWA MUDA AMBAPO MADUKA YALIFUNGWA, BIASHARA ZILISIMAMA KWA MUDA KTK MITAA YA MAKOROBOI NA SEHEMU KTK BARABARA YA NYERERE MADUKA YALIFUNGWA HUKU WANANCHI WAKIHAHA KUKIMBIA HUKU NA HUKO ALIMURADI TU KUTOWEKA ENEO LA TUKIO KWANI HATA WALE AMBAO WALIKUWA NDANI YA DALADALA NA VYOMBO VINGINE VYA USAFIRI VILIVYOKUWA VIKINGOJA RUKSA YA TAA ZA BARABARANI KTK BARABARA YA NYERERE ILIWALAZIMU KUSHUKA KUKIMBIA KUTAFUTA PA KUJISITIRI.

SABABU KUBWA YA YOTE HAYA NI LILE ZOEZI LA KAMATA KAMATA SAFISHA JIJI LINALOFANYWA KAMA ADA NA MGAMBO WA JIJI DHIDI YA MACHINGA WANAOCHUUZA BIDHAA NDOGONDOGO IWE KWA KUTEMBEZA AU KWA KUTANDAZA BIDHAA KATIKA MITAA YA JIJI LA MWANZA.

SHESHE LILIANZA PALE MGAMBO WALIPO KAMATA MALI ZA MOJA WA MACHINGA AMBAYE ALIKUWA AKICHUUZA BIDHAA ZAKE PALE KTK MITAA MAARUFU YA KIBIASHARA MAKOROBOI...
MACHINGA KATU HAKUKUBALI MALI ZAKE ZIENDE "AMA ZANGU AMA ZAO LABDA KAMA MGAMBO WANASAIDIA KULISHA FAMILIA YANGU" MACHINGA HUYO ALISIKIKA AKISEMA.

HATUA CHACHE MVUA YA MAWE IKAANZA NA KUONGEZEKA KADRI MUDA UKISONGA, WAFANYABIASHARA WADOGO WAKE KWA WAUME WAKIWARUSHIA MAWE MGAMBO HAO KUWAONDOA WASIWABUGHUDHI KATIKA VIUNGA VYAO VYA KUJITAFUTIA.

POLISI KUONA HALI IMEZIDI KUWA TETE, WAKACHUKUA JUKUMU LA KUFYATUA RISASI HEWANI, RISASI KADHAA ZIKALIA MWISHO WA SIKU PILISI WAKAFANIKIWA KUTAWANYA WAFANYABIASHARA HAO NA KUKAMATA KADHAA WANANAOTUHUMIWA KUHUSIKA NA VURUGU HIZO.

UHARIBIFU:
KIOO CHA GHOROFA YA KWANZA CHA JENGO JIPYA LA SEIF PLAZA KIMEPUPUTIKA MARA BAADA YA KUTOBOLEWA NA RISASI NA KAMA KUNGELIKUWA NA MTU AKIFUATILIA YALIYOKUWA YAKITOKEA KTK VURUGU HIZO TUNGEKUWA TUNAZUNGUMZA MENGINE.

HALI YA SASA NI TULIVU,
SHUGHULI ZINAENDELEA KAMA KAWAIDA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.