ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 28, 2009

KWA MARAFIKI WOTE EID MUBARAK


MARAFIKI KAJUA KANAENDA KUZAMA NA LEO NDIYO SIKUKUU NAMI NAWATAKIA EID NJEMA INSHAHLAH MSHEREHEKEE VYEMA

WAWILI KATI YA MAELFU YA MARAFIKI ZANGU KUSHOTO DJ ELLY THE BIG DADDY 4BY4 aka MTUMBA WA CLOUDS FM DAR (DJ WA KIPINDI KWA RAHA ZETU, NITE KALI NA BAMBATAA) NA DJ ALLY MZEE WA KITU JUU YA KITU TOKA CLOUDS FM ARUSHA.

Friday, November 27, 2009

FLASH BACK PICTURE NA HAYATI DJ BUSH DOCTOR


TAKRIBANI WIKI KADHAA SIKUKULETEA MZIGO SAMPULI HII KUENZI ZAMA ZA KALE LAKINI LEO MZIGO HUU HAPA

TOFAUTI NA MIAKA YA SASA AMBAPO KUNA MITINDO MINGI HALI INAYOPELEKEA MINGINE YAWEZA KUKUPITA HATA USIIONE AU KUHUSIKA NAYO (kuitumia aka kutumika nayo), MIAKA YA ZAMANI MITINDO YA NYWELE, MAVAZI NA VIATU YOTE KWA PAMOJA IKIWA KATIKA STYLE MOJA ILIKUWA IKISAMBAA KWA KASI NAKUTAMBULIKA KOTE NCHINI KAMA "MTINDO WA WAKATI" SABABU KUBWA NI KWAMBA TULIKUWA NA WABUNIFU WACHACHE TENA WALIO WAUKWELI MBALI NA HIVYO PIA SERA ZA "UMOJA" NAZO ZILICHANGIA TOFAUTI NA LEO KUNA MADIZAINA WAKUMWAGA NA SERA TULIZO NAZO NI ZA "UDIFERENTI" KILA MTU ANATAKA KUONEKANA TOFAUTI.
MCHEKI KUSHOTO BROTHER MWITA VSS NA MKALI WA KUGONGA MAWE ENZI HIZO DJ BUSH DOCTOR KULIA MA SUSPENDER NA MAMBO YA KUMECHISHA JUU MPAKA CHINI, KITAMBAA KILIKUWA DALAZ NINI?

Thursday, November 26, 2009

HOMA YA MAFUA YA NGURUWE YAINGIA MWANZA




WAKATI TAIFA LA TANZANIA LIKIENDELEA KUJIPANGA NA KUJIZATITI KATIKA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA HOMA KALI YA MAFUA YA NGURUWE MKOA WA MWANZA UMETHIBITISHA KUINGILIWA NA UGONJWA HUO HATARI.
AKIZUNGUMZA LEO HII OFISINI KWAKE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MGANGA MKUU WA MKOA WA MWANZA DR.MESHARK MASSI AMESEMA KUWA UGONJWA HUO AWALI ULIGUNDULIKA KATIKA KIJIJI ILULA WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA AMBAPO WANAFUNZI 56 WA SHULE YA MSINGI ILULA WALIONEKANA KUWA NA DALILI MBALIMBALI ZA UGONJWA HUO.
MARA BAADA YA HAPO IDARA YAKE YA AFYA WILAYA ILITUMA TIMU YA WATAALAMU KUCHUNGUZA HALI, KUPATA VIPIMO NA SAMPULI NDIPO MAJIBU YAMETOKA HII LEO KUBAINISHA KUWA JUMLA YA WATU 142 WAMEATHIRIKI NA UGONJWA HUO IKIWA NI WANAFUNZI, WAALIMU NA BAADHI YA WANAKIJIJI WA ILULA WILAYANI KWIMBA.
KATIKA HALI HIYO MGANGA MKUU HUYO WA MKOA WA MWANZA AMETOA WITO KWA WANANCHI WA KIJIJI HICHO NA VIJIJI JIRANI KUCHUKUA TAHADHARI ZINAZOSTAHILI KUJIKINGA NA MARADHI HAYO IKIWA NI PAMOJA NA KUNAWA MIKONO KWA SABUNI NA MAJI SAFI MARA KWA MARA, VILEVILE KUEPUKA KUWA KUWA KARIBU NA MTU MWENYE DALILI ZA UGONJWA HUO
AIDHA DR. MASSI AMEWAASA WANANCHI KUZUIA MDOMO NA PUA KWA KITAMBAA LAINI / TISSUE WAKATI WA KUKOHOA NA KUPIGA CHAFYA, KUFUATA KANUNI ZOTE ZA AFYA NA KWA WAFUGA NGURUWE KUZINGATIA DALILI ZA UGONJWA KWA NGURUWE NA KUEPUKA KUGUSANA NA MIFUGO HIYO IWAPO ITAONEKANA KUWA NA DALILI ZINAZOTAJWA NA WAELIMISHAJI.
SHANGWE LILILIPUKA TOKA KWA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA MGANGA MKUU HUYO KUNENA KWAMBA "UGONJWA WA MAFUA YA NGURUWE HAUAMBUKIZWI KWA KULA NYAMA YA NGURUWE ILIYOPIKWA" HATA RAFIKI YANGU ..... ALISHANGILIA. HATA HIVYO INATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI WA MAANDALIZI NA KABLA NYAMA HAIJAPIKWA.
MPAKA SASA HAKUNA TAARIFA ZOZOTE ZA MGONJWA WA MARADHI YA MAFUA YA NGURUWE ALIYERIPOTIWA KUFARIKI DUNIA MKOANI MWANZA.
SHULE YA ILULA IMEFUNGWA TANGU TAREHE 19 NOVEMBER 2009 MARA TU BAADA YA WANAFUNZI WA SHULE HIYO KUGUNDULIKA KUWA NA DALILI ZA UGONJWA HUO.

MIE NIMESAJIRI VIPI MWENZANGU?


MAMLAKA YA MAWASILIANO IMERONGA SANA KUHUSU HILI MWISHO WA SIKU WENYE SAUTI ZAO (WAIMBAJI) NAO WAKATUMIKA KUHAMASISHA HIMA TUKASAJILI NAMBA ZETU, TUME IMESHANENA KUWA KITAKACHOFUATA NI KUZIFUNGIA ZISIPATE MAWASILIANO NAMBA AMBAZO HAZITAKUWA ZIMESAJIRI IFIKAPO MWISHO WA MWEZI HUU...... SASA WA TZ WENGI TU MATOMASO.. AAAAH HAITOWEZEKANA.....SUBIRINI MUWE MFANO KUDADADEKI!

Tuesday, November 24, 2009

BORA TUWEKE SAMAKI


IMEZOELEKA NA IMEKUWA DESTURI KUONA SANAMU NYINGI ZISIMIKWAZO HAPA NCHINI ZIKIWA NA TASWIRA ZA MOJA YA VIONGOZI WETU WENYE HISTORIA KTK HARAKATI ZA MAENDELEO YA NCHI AU ENEO HUSIKA LAKINI SASAAAA! SHUHUDIA HIKI KIPITA SHOTO CHA KAUMA KILICHOPO BARABARA YA KENYATA JIJINI MWANZA KATIKA MWONEKANO MPYA WA MOJA YA UTAMBULISHO WA ZAO LINALOPATIKANA ZIWA VICTORIA HUYU NI SAMAKI AINA YA SATO. NAJUA UNASWALI...ULIZA

Monday, November 23, 2009

MPANGO KAMILI WA SHEA YAKO


KAULI MBIU YA FIESTA 2009 ONE LOVE KWA KIASI KIKUBWA IMEFANIKIWA KUUNGANISHA MATUKIO HUSIKA SHUGHULINI NA HISIA ZA WATU, KWAMBA YALE YALIYOAHIDIWA NDIYO YALE YALIYOTOKEA LABDA PENGINE TUSEME ZAIDI..... NANI ANABISHAA!! PICHA ZAIDI tembelea www>michuzijr>blogspot>com


NIFIESTA PEKEE CHEKSHIA TAIFA LINAVYOTANGAZWA


WHAT NEXT?