ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 24, 2009

NASMA HATUKO NAYE TENA

NASMA HAMISI KIDOGO NDIVYO ALIVYOKUWA AKITAMBULIKA, NI MMOJA WA WASANII WALIO ITENGENEZA HISTORIA YA MAPINDUZI YA MUZIKI WA TAARABU HAPA NCHINI. AKIZALIWA MIAKA 57 ILIYOPITA KILWA KIVINJE AMEFARIKI DUNIA KWA HOMA YA MARALIA USIKU WA KUAMKIA JUMAPILI YA WIKI HII. ALIWAHI KUFANYA KAZI NA TANZANIA ONE THEATRE (SASA TOT PLUS) MWAKA 1993. KISHA AKJIUNGA NA MAHASIMU WAKUBWA WA TOT ENZI HIZO MUUNGANO CALTURAL TROUPE AMBAKO ALISHIRIKI KUIMBA NYIMBO MBALIMBAKI LAKINI ZILIZO MPA UMAARUFU ZAIDI NI KAONA MAMBO IKO HUKU NA SANAMU LA MICHELIN. ALISHASHIRIKI PIA KUUNAKSHI MUZIKI WA KIZAZI KIPYA KWA KUSHIRIKIANA NA INSPEKTA HAROON KWENYE SINGLE YAKE WAPE VIDONGE VYAO. HALI ILIYOWASTAAJABISHA WENGI "KHAA KUMBE INAWEZEKANA?" HAKIKA HILI NI PENGO MUNGU ILAZE PEMA ROHO YA MAMA YETU AMEN.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.